LONDON, England

ASTON VILLA wakiwa nyumbani hawatamsahau mshambuliaji wa klabu ya Leeds United, Patrick Bamford kwa kuwatungua (hat-trick), kwenye mchezo wa ligi kuu England wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Mabao ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 yalipachikwa dakika ya 55, 67 na 74 na kuwafanya Leeds kuondoka na pointi tatu Uwanja wa Villa Park na kuwafanya Villa wapoteze mchezo wao wa kwanza kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa walikuwa wamecheza mechi nne bila kupoteza.

Matokeo hayo yanaifanya Aston Villa kuwa nafasi ya pili na pointi zake 12 huku Leeds ikiwa nafasi ya tatu na pointi 10 baada ya kucheza mechi sita ndani ya ligi kuu England, ambayo imeanza kwa kasi kubwa msimu huu.