TOKYO,JAPANI

BARAZA la Sayansi la Japani liliamua kumsihi Waziri Mkuu wa Japani Suga Yoshihide, aelezee sababu za kukataa kuwateua watu sita kuwa wanachama wapya wa bodi inayoongoza ya elimu, na lilifufua upya ombi la uteuzi wao.

Baraza hilo limetengwa kama shirika maalumu chini ya mamlaka ya waziri mkuu, lakini linatoa mapendekezo huru ya kisera.

Baraza hilo liliwasilisha orodha ya wateule 105 kujiunga na baraza hilo tangu Alhamisi iliyopita,lakini Suga alikataa wateule sita miongoni mwao.

Watendaji wa baraza hilo walikutana na kuamua kumuomba Suga kuelezea sababu za kukataa kwake na kuidhinisha haraka uteuzi wa wateule hao.

Ombi hilo liliwekwa kwenye mtandao wa baraza hilo, na kuwasilishwa kwa Suga kupitia kitengo husika cha Serikali.

Rais wa baraza hilo,Kajita Takaaki ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Nobeli na Profesa wa heshima kwenye Chuo Kikuu cha Tokyo, alisema baraza hilo haliwezi kushughulikia suala hilo bila ya kujua sababu za kukataliwa kwa wateule hao.