NA KHAMISUU ABDALLAH

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimeongoza katika majimbo tisa ya wilaya ya Mjini kunzia ngazi ya Uwakilishi, Ubunge na Udiwani.

Majimbo hayo ni pamoja na Jimbo la Malindi, Mpendae, Kikwajuni, Kwahani, Shaurimoyo, Chumbuni, Magomeni, Amani na Jimbo la Jang’ombe.

Akitangaza matokeo katika skuli ya Dk. Ali Mohamed Shein Msaidizi Ofisa Uchaguzi wilaya ya Mjini Ali Khamis Mohammed kwa jimbo la Kikwajuni kwa nafasi ya Uwakilishi ilishikiliwa na Nassor Salim Ali aliepata kura 9,586, akifatiwa na Hamad Mussa Yussuf wa ACT Wazalendo 1884, huku Hamadi Masauni kuwa mbunge mteule aliepata kura 8218, akifuatiwa na Ramadhan Yakuti wa ACT wazalendo aliepata kura 1924.

Kwa upande wa jimbo la Jang’ombe alioongoza na Ali Abdulgulam Hussein aliongoza kwa kura 8,999 na Abdalla Ali Abdalla wa ACT Wazalendo 1,402 sawa na asilimia 13.3 huku nafasi ya Ubunge ikishiliwa na alieengoza kwa kura Ali Hassan Omar (King), alitangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo alieongoza kwa kura 7617 akifuatiwa na Yusuf Maalim wa ACT Wazalendo aliepata kura 1966.

Jimbo la Mpendae alisema alieongoza kwa nafasi ya Uwakilishi alikuwa ni Shaban Ali Othman wa CCM aliepata kura 6,518 sawa na asilimia 70 akifatiwa na Ali Hamad Ali kutoka chama cha ACT Wazalendo aliepata kura 2,545 sawa 27.3 na ubunge Mpendae, mgombea wa CCM Taufik Salum Turky alitangazwa mshindi alieshinda kwa kura 5,529 akifuatiwa na Suleiman Ali wa ACT wazalendo aliepata kura1,936.

Kwa upande wa Jimbo la Shaurimoyo msimamizi huyo alimtangaza Hamza Hassan Juma wa CCM aliongoza kwa kura CCM aliongoza kwa kura 8,509 sawa asilimia 75. 5 na Abdalla Sadala Boi wa ACT Wazalendo alipata kura 2,408 sawa na 21.4 huku nafasi ya Ubunge alimtangaza mgombea wa CCM Ali Juma Mohammed kuwa ni mshindi wa jimbo hilo, aliepata kura 8792 akifuatiwa na Maua Mohd kupitia chama cha ACT Wazalendo aliepata kura 1799.

Jimbo la Kwahani uwakilishi alieongoza alikuwa ni Yahya Rashid Abdalla wa CCM aliongoza kwa kupata kura 6,934 sawa asilimia 83.3 na Omar Mussa Makame wa ACT Wazalendo alipata kura 1,316 sawa na asilimia 15 huku nafasi ya Ubunge Ahmed Yahya Abdulwakil, kupitia tiket CCM alieshinda kwa kura 6222, akifuatiwa na Issa Vuai wa ACT Wazalendo aliepata kura 1143.

Jimbo la Malindi aliongoza kwa nafasi ya Uwakilishi alikuwa ni Mohammed Ahmada Salum wa CCM aliepata kura 7,764 sawa na asilimia 65.8 akifatiwa na Ismail Jussa Ladhu wa ACT Wazalendo aliepata kura 3,726 sawa na asilimia 31.6 huku nafasi ya Ubunge Mohammed Suleiman Omar wa CCM aliongoza kwa kura 7,807 akifuatiwa na Halima Ibrahim Mohd wa ACT wazalendo, aliepata kura 3,259.

Msimamizi huyo alibainisha kwamba kwa jimbo la Chumbuni aliongoza Miraji Khamis Mussa wa CCM aliongoza kwa kura 8,604 sawa na asilimia 76.7 na Haroub Mohammed Sindano wa Chama cha CHADEMA alipata kura 2,111 sawa na asilimia 18 huku nafasi ya Ubunge ikishikiliwa na Ussi Salum Kondeza kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM aliepata kura 7379, akifuati wa na Mrisho Abama wa ACT Wazalendo aliepata kura 2221.

Jimbo la Magomeni ngazi ya Uwakilishi Jamal Kassim Ali wa CCM aliongoza kwa kupata kura 7,144 sawa na asilimia 72.2 na Bakar Juma Omar wa ACT Wazalendo alipata kura 2,209 sawa na asilimia 22.3 huku nafasi ya Ubunge ikichukuliwa na Mwanakhamis Kassim Said, kupitia Chama cha mapinduzi alieoongoza kwa kura 6129, akifuatiwa na Dude Haji wa ACT wazalendo aliepata kura 2122.

Kwa upande wa Jimbo la Amani Rukia Omar Ramadhan wa CCM aliongoza kwa kura 6,850 sawa 75.6 na Mohammed Khamis Mohammed ACT Wazalendo alipata kura 1,947 sawa na asilimia 21.5 huku nafasi ya Ubunge Mussa Hassan Hussa wa CCM kuwa ni mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 5122, akifuatiwa na Khamis Silima wa ACT Wazalendo aliepata kura 1708.