NA HUSNA SHEHA NA MWAJUMA MMANGA

MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Wilaya Magharibi ‘A’ katika Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Hidaya Mrisho, amemtangaza Zubeda Khamis, Shaib kuwa Mbunge wa jimbo la Mfenesini, baada ya kupata kura 7,785, na kumshinda mpinzani wake Raisa Abdalla Mussa wa ACT Wazalendo kwa kupata kura 1539.

Msimamizi huyo pia amemtangaza Abdulghafar Idrissa Juma CCM kuwa mshindi wa ubunge jimbo la Mtoni kwa kupata kura 9468, na kuwashinda wapinzani wake Juma Khamis Juma wa ACT Wazalendo aliyepata kura 3008, kati ya kura 12,899 zilizopigwa.

Vile vile alimtangaza Mwantakaje Haji Juma kuwa mbunge wa jimbo la Bububu aliyepata kura kura 9497 kwa kumshinda mpinzani wake Faki Haji Makame wa ACT Wazalendo aliyepata kura 1546.

Katika jimbo la Welezo, Maulid Saleh Ali wa CCM ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 7307 na kumshinda mpinzani wake Saleh Mohammed Saleh wa ACT wazalendo alityepata kura 2551.

Nalo jimbo la Mwera ametangazwa Zahor Mohammed Haji wa CCM aliyepata kura 6945 na kumshinda mpinzani wake Ame Khamis Ame wa ACT Wazalendo aliyepata kura 2531.

Nae msimamizi wa uchaguzi wa wilaya hiyo Suluhu Ali Rashid amemtangaza Mihayo Juma Nunga kuwa Mwakilishi mteule wa jimbo la Mwera kwa kupata kura 6331 na kuwashinda washindani wake Nassor Ahmed Mazrui wa ACT Wazalendo amepata kura 2944.

Suluhu pia alimtangaza Machano Othman Said kuwa Mwakilishi wa jimbo la Mfenesini kwa kupata kura 8250 na kuwashinda washindani wake Suleiman Mohammed Bakar wa ACT Wazalendo kupata kura 266, jimbo la Bububu alitangazwa mwakilishi wa jimbo hilo Mudrik Ramadhan Salum amepata kura 7380na jimbo la Welezo ameshinda Hassan Khamis Hafidh amepata kura 8135.  Nae mwakilishi wa jimbo la Mtoni Huseein Ibrahim Makungu ‘Bhaa’ ameteuliwa kuwa mwakilishi kwa kuwa hana mpinzani.