LONDON, England

IMERIPOTIWA kuwa Chelsea ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya Paulo Dybala anayekipiga ndani ya kikosi cha Juventus.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 raia wa Argentina amekuwa nje ya mpango wa kocha mkuu wa Juventus, Andrea Pirlo kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kusumbuliwa na majeraha hivi karibuni. 

Kwa mujibu wa Tutto Mercato Web, imeripoti kwamba Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea ametajwa kuhitaji  saini ya nyota huyo ili awe ndani ya kikosi hicho.

Uhitaji wa saini ya Dybala unaongezeka baada ya timu hiyo kukosa saini ya Lautaro Martinez msimu huu, jambo ambalo linawafanya wafikirie kumpata mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja.