BEIJING, CHINA

China imesema kuwa Marekani inatishia amani katika eneo la mipaka ya bahari ya Taiwan, baada ya meli ya kivita ya Marekani kuingia kwenye eneo hilo katika wakati ambapo mvutano unaongezeka baina ya Beijing na Taipei.

Msemaji wa kamanda wa jeshi la majini la China Zhang Chunhui, alisema waliifuatilia kwa karibu meli hiyo iitwayo USS Barry wakati ilipofanya safari yake kwenye mipaka ya bahari ya Taiwan.

Jeshi la Majini la Marekani limeitaja safari hiyo kuwa ya kawaida kwenye eneo hilo la bahari.Zhang amesema Marekani inapaswa kukomesha maneno na vitendo vyake vya kichokozi kwenye eneo hilo na kuongeza kuwa China iko tayari kulinda mipaka yake na kusimamia amani na utulivu wa mipaka ya bahari ya Taiwan.