BEIJING,CHINA      

CHINA imepitisha sheria ya kuimarisha udhibiti wa usafirishaji nje wa bidhaa zinazohusiana na usalama wa taifa.

Hatua hiyo inaonekana kama mwitikio wa hatua za Marekani dhidi ya makampuni ya China.

Shirika la habari linaloendeshwa na Serikali ya China la Xinhua limeripoti kuwa Kamati ya kudumu ya Bunge la watu wa China imeidhinisha sheria hiyo.

Sheria hiyo itaanza kutekelezwa Disemba Mosi,ikizuia na kudhibiti usafirishaji wa bidhaa,teknolojia na huduma zinazohusiana na usalama wa taifa kwenda nje ya nchi hiyo.

Sheria hiyo itayalenga makampuni yanayotegemea mitaji ya kigeni na vyombo vyengine vinavyoweza kuhatarisha usalama wa China.

Kwa sasa, bado haipo wazi ni vipengele vipi mahususi vitakuwa chini ya sheria hiyo.

Sheria hiyo pia itadhibiti usafirishaji nje wa bidhaa zilizotengenezwa nje ya China kwa kutumia rasilimali zilizoagizwa kutoka nchini humo.