BEIJING,CHINA

CHINA zinaendelea na mazungumzo ya kurejesha safari za kibiashara kati ya nchi hizo mbili kuanzia mapema mwezi huu.

Serikali ya Japani taratibu iliregeza masharti ya kuingia nchini humo yaliyokuwa yakitekelezwa ili kuzuia ueneaji wa virusi vya corona.

Tayari imerejesha safari za kibiashara na Korea Kusini,Singapore na nchi nyengine.

Vyanzo vya habari serikalini vinasema maofisa wanajadili namna ya kushughulikia matokeo ya upimaji wa virusi vya corona kwa kuwa Japani na China zinatumia njia tofauti za upimaji kwa wasafiri wanaoingia katika nchi hizo.

Mwaka jana,China ilikuwa na wasafiri wengi wa kibiashara waliofika Japani ambao ni karibu 370,000.

Serikali ya Japani inatumai kurejesha safari za kibiashara na China hivi karibuni ili kufufua uchumi.