DORTMUND, Ujerumani
KLABU ya soka ya Borussia Dortmund imeahirisha mkutano wake mkuu wa mwaka wa wanachama kwa muda usiojulikana kutokana na janga la virusi vya ‘corona’.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika Novemba 22, lakini, rais wa Borussia Dortmund, Reinhard Rauball, amesema katika taarifa ya klabu hiyo kuwa na wanachama wengi iwezekanavyo katika tukio hilo hakuwezekani kutokana na vizuwizi, na mkutano kwa njia ya video hauwezekani pia katika mwaka 2020.

“Kukiwa na karibu wanachama 160,000 wa BVB, kwa bahati mbaya hakuna njia ya teknolojia ya kufanya mkutano kama huo kwa njia ya video katika hali ya inayokubalika”, alisema.
“Binafsi nasikitika kwa hili, kwa kuwa mawasiliano ya moja kwa moja nanyi, wanachama wetu, ni muhimu kwetu”.
Mkutano wa wadau wa Dortmund kwa wakati huu utafanyika kwa njia ya mtandao, Novemba 19, limesema gazeti la Kicker.(AFP).