PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay amekubali kuingia mkataba na Barcelona na huenda akajiunga na timu hiyo katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, kulingana na mkurugenzi wa Ufaransa Juninho.
Mchezaji huyo wa zamani wa man United mwenye umri wa miaka 26 aliwachwa nje katika kikosi cha timu ya kwanza ya Lyon siku ya jumapili iliotoka sare na Marseille.
Amekubaliana na Barcelona , hilo hatuwezi kuficha hata kidogo, alisema Juninho. Wakati huohuo beki Eric garcia anaweza kujiunga tena na Barcelona kutoka Manchester City.
Timu hiyo ya ligi kuu ingemruhusu kinda huyo kurudi iwapo itapokea ombi la uhakika , lakini pia wamejiandaa kumwachilia raia huyo wa Uhispania kuondoka katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao.
Garcia ni mchezaji huru baada ya makataba wake kukamilika msimu uliopita na ameambia City kwamba hatotia saini mkataba mwengine.
Wakati huohuo mchezaji wa Lyon Depay amefunga magoli 58 katika mechi 144 tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Ligue 1 kutoka Manchester United 2017.
Depay alikuwa na wakati mgumu katika ligi ya England akiichezea United baada ya kusainiwa na Lousi van Gaal kwa dau la pauni milioni 31 mwaka 2015 , akifunga magoli 7 katika mechi 53.
Iwapo Depay atakamilisha uhamisho huo atashirikiana aliyekuwa mkufunzi wa Uholanzi Ronald Koeman , ambaye alichukua uongozi wa Barcelona msimu huu.