FRANKFURT, Ujerumani
WAENDESHA mashtaka wa Ujerumani wamefanya upekuzi katika makao makuu ya ofisi za Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) pamoja na nyumba za wajumbe wa chama hicho kufuatia uchunguzi wa udanganyifu wa kukwepa kulipa kodi.

WAENDESHA mashtaka mjini Frankfurt wamesema makao makuu ya Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) ambalo ni moja kati ya mashirikisho makubwa pamoja na nyumba za maofisa wa DFB zimepekuliwa kwa tuhuma za kukwepa kodi.

Msako huo ulifanywa katika majimbo matano kote Ujerumani ambayo ni Hesse, Bavaria, North-Rhine Westphalia, Lower Saxony na Rhineland-Palatinate.
Takriban maofisa 200 walishiriki katika zoezi hilo na miongoni mwao wakiwa maofisa wa kukusanya ushuru na maofisa wa polisi.

Uchunguzi umeelekezwa kwa kiasi kikubwa dhidi ya maofisa watendaji sita wa zamani au wa sasa wa DFB. Wanashutumiwa kwa kutangaza kimakosa kwa makusudi mapato ya matangazo katika mwaka 2014 na 2015 kwenye michezo ya nyumbani ya timu ya taifa. Mashtaka hayo yanahusiana na matangazo ya mzunguko katika viwanja vya michezo.

Maofisa wa polisi wakiwa wamesimama nje ya ofisi za makao makuu ya DFB, kufuatia tangazo kwamba polisi imevamia ofisi na makaazi wa wanchama wa juu, kuhusiana na uwezekano ukwepaji mkubwa wa kodi, Oktoba, 07, 2020.

Inaarifiwa kuwa kiasi cha ushuru kilichokwepwa kinaweza kuzidi euro milioni 4.7.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika shirikisho hilo, uchunguzi unaashiria watuhumiwa hao walifahamu kulikuwa na shaka katika marejesho, lakini, hawakuchukua hatua kwa lengo la kuipatia DFB faida kubwa ya ushuru.


Hata hivyo watu hao sita hawakutajwa. Hii ndio kesi ya hivi karibuni katika mfululizo wa kesi za kisheria ambazo chama kikubwa cha mpira wa miguu kimepatikana katika siku za hivi karibuni.
Awali uchunguzisawia na huo ulifanywa wakati wa Kombe la Dunia la 2006 kwa Ujerumani na jinsi fedha zilivyotumiwa katika kuelekea mashindano hayo.

Hivi karibuni DFB ilifikisha mwisho ushirikiano wake na wakala wake wa uuzaji baada ushirikiano wa takriban miaka 40 baada ya ripoti kuibuka kwa makosa ya kifedha.(AFP).