NA MWANAJUMA ABDI, D AR ES SALAAM

MGOMBEA wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli amesema ana deni kubwa kwa wananchi wa jiji la Dar es Salaam.

Dk. Magufuli alieleza hayo jana katika viwanja vya Tanganyika Packers, alipokuwa akifunga kampeni katika jiji hilo, ambapo alitumia fursa hiyo kujiombea kura na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM.

Alisema mahudhuria makubwa ya wananchi wa Dar es Salaam katika mkutano huyo yamemfanya kubaini kuwa ana deni, ambapo atawalipa kwa kuwaletea maendeleo baada ya ushindi kwenye uchaguzi wa Oktokab 28 mwaka huu.

Kwa upande wa nchini Tanzania, alisema Nyerere amewaachilia watazania mambo matano ikiwemo kupigania uhuru ambao umewawezesha wananchi kuwa na taifa lao na kujiamulia mambo yao.

Alisema  jambo la pili aliloliacha baba wa taifa ni amani na utulivu, hiyo ni tunu kubwa waliyoashiwa, ambapo katika kipindi chote cha uhai wa Nyerere alipigania amani ndani na nje ya mikapa ya nchi.

Alisema suala la tatu alililoachwa na Nyerere ni umoja na mshikamano wa taifa hili, ambapo pamoja na nchi kuwa na makabila 121, lakini wanaunganishwa na utanzania wao pamoja na lugha ya kiswahili.

Alisema suala jengine ni muungano aliouasisi kwa kushirikiana na marehemu sheikh Abeid Amani Karume ambao umwezesha kuundwa kwa nchi yenye nguvu.

Alisema suala la tano ambalo baba wa taifa alilisimamia ni kujenga Taifa la kujitegemea hususani kwa kutumia juhudi na rasilimali za Tanzania aliwahi kusema ‘hatuna budi kujenga nchi hii kwa kujitegemea kwa kutumia rasilimali tulizonazo’, alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika nafasi zote za urais, ubunge na udiwani, sambamba na wanakawe kuwataka wamchaguwe Askofu Gwajima ili waweze kuibadilisha kawe kwa maendeleo iliyoachwa nyuma kwa miaka 10 sasa.