NA ASYA HASSAN

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA Zanzibar), imesema waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wanahitaji kuelimishwa, ili waweze kufika mahakamani kutoa ushahidi juu ya kesi hizo.

Ofisa tathmini na ufatiliaji kutoka chama hicho, Mohammed Khatib Mohammed, alisema hayo alipokuwa katika kikao cha pamoja na wanamtandao kutoka Mikoa mitatu ya Unguja wanaofatilia vitendo vya udhalilishaji.

Alisema tatizo kubwa liliyopo katika kesi hizo ni waathika kutofika mahakamani kutoa ushahidi, hivyo elimu itasaidia kuwahamasisha na kuweza kujiamini kusimama imara katika kutetea na kudai haki zao.

Afisa huyo alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Finland wanasimamia mradi wa kuwasaidia walioathirika na vitendo vinavyotokana na ngono, ili waweze kufika mahakamani kutoa ushirikiano wa matendo hayo.

Alisema vitendo vya udhalilishaji ni vya aibu na vimekuwa vikiwafanya waathirika kushindwa kufatilia kesi hizo kwa kuhofia suala hilo pamoja na kunyanyapaliwa.

Baadhi ya wanaharakati wanaofatilia vitendo hivyo walisema jamii inahitaji kuelimishwa, ili waweze kuondosha muhali juu ya kupambana na vitendo hivyo kwani mshtakiwa hawezi kutiwa hatiani bila kupatikana ushahidi.