ZASPOTI
MENEJA wa zamani wa Ismaily, Muhsin Ertugral, amemshauri meneja mpya wa Al Ahly, Pitso Mosimane, kabla ya kipindi chake cha kwanza katika moja ya ligi zenye ushindani mkubwa Afrika.
Ertugal alikuwa na kipindi kifupi na Ismaily nyuma mnamo 2005 kabla ya kurudi Afrika Kusini na Ajax Cape Town na alibakia nchini tangu wakati huo.


Katika kipindi hicho alipata nafasi ya kukutana na Mosimane mara kadhaa kwenye mashindano ya ndani.
Kufuatia kutangazwa kwa uhamisho huo, Ertugal alimsifu mwenzake akisema kwamba anastahili. Lakini akamwambia kwamba lazima aonyeshe matokeo ya haraka.


“Anastahili kuwa huko na kuwepo na kuitunza itakuwa changamoto kwake. Ana wachezaji wazuri ambao wanataka kufikia mafanikio. Ana zaidi ya nusu ya wachezaji katika timu ya taifa ya Misri na inamfanya iwe rahisi zaidi”, Ertugral aliambia tovuti ya Afrika Kusini ya Phakaaathi.


“Hakuna uvumilivu kabisa juu ya hilo katika klabu ulimwengu, lazima utoe kama ilivyokuwa jana. Jambo muhimu zaidi ni kwamba anapaswa kubadilika haraka iwezekanavyo. Hakuna uvumilivu hata kidogo, hakuna chochote chini ya kushinda taji na Ligi ya Mabingwa ya Caf. Alichukua changamoto na anajua kinachotarajiwa.


Mosimane pia atapata fursa ya kuchukua mara moja taji jengine la Ligi ya Mabingwa CAF kwani Mashetani Wekundu hao kwa sasa wapo katika nusu fainali ambapo watapambana na Wydad Casblanca.
Ertugral anaamini kwamba inawezekana yeye kufikia kazi hiyo, lakini, haitakuwa kazi rahisi.


“Hakuna kinachokuja kwa urahisi, yote ni kutokana na bidii yake na watu wengi hawajui ni muda gani makocha hutumia kufanikiwa. Kwa kweli hii itakuwa changamoto kubwa katika kazi yake. Nina hakika kabisa kwamba baada ya mabadiliko ya haraka atafanikiwa na Al Ahly”, alieleza.


“Nina imani kuwa ana vifaa na anajua jinsi ya kushughulikia vyombo vya habari kwa sababu ni nchi ambayo ina mahitaji yake kutoka kwa vyombo vya habari. Wachezaji pia wanahitaji maelezo kadhaa ili waweze kujua jinsi anavyotarajia watatumbuiza uwanjani”.


Meneja huyo mwenye umri wa miaka 56 pia anaweza kushinda mataji matatu kwani Kombe la Misri bado linashiriki baada ya mashetani wekundu hivi karibuni kufuzu robo fainali.
Mchezo wake wa kwanza akiwa madarakani na Al Ahly ulitarajiwa kupigwa dhidi ya Arab Contractors.
Kocha huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns anachukua nafasi ya raia wa Uswisi, Rene Weiler ambaye aliachana na miamba hiyo ya jijini Cairo.


Mosimane alitumia miaka minane ya mafanikio na Wabrazil hao na alibeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016.(Goal).