ZASPOTI

MIAMBA ya Tunisia ya Esperance Sportive de Tunis na matajiri wa Al Ahly, wanaripotiwa kumfukuzia mshambuliaji wa El-Gouna raia wa Zambia,Walter Bwalya.
El Gouna ilimsaini Bwalya mwanzoni mwa msimu akitokea Nkana FC ya Zambia na licha ya kuanza polepole, anacheza sehemu kubwa katika mapambano ya kutoshuka daraja kwa timu yake.
Mchezaji huyo mwenye wa miaka 25 alifunga tu magoli matatu kati ya Septemba 2019 na Machi 2020. Hata hivyo, alijikomboa tangu kuanza kwa ligi mnamo Agosti alipocheka na nyavu mara tisa katika mechi 14.

Maonyesho yake yalionekana kuvutia idadi kubwa ya wahusika wa hali ya juu wakiwemo wababe wa Afrika Esperance Sportive de Tunis na Al Ahly.
Kulingana na gazeti la Tunisia, Essahafa, Esperance wanatafuta kufufua ushambuliji wao. Klabu hiyo tayari ilitangaza kuondoka kwa Junior Lokosa wa Nigeria na wanaangalia kumtema, Ibrahim Ouattara.
Hata hivyo, inaonekana kwamba damu na dhahabu sio peke yao wanaopendezwa na Bwalya kwani Al Ahly, ambao wanajulikana kuwa na uhusiano mzuri na bodi ya El-Gouna, wanatafuta kumnyakua.


Kwa sasa Bwalya amebakiza michezo miwili kwenye Ligi Kuu ya Misri na El-Gouna. Atatarajia kuwa na athari katika changamoto hizi mbili za mwisho kwani ni muhimu kwa uhai wa klabu.(Goal).