KATIKA safu yetu hii ya tiba leo hii tutauangazia mchaichai na faida yake katika mwili wa binaadamu.
MCHAICHAI ni aina ya majani upandwao kwa ajili ya mahitaji ya
binadamu, asilimia kubwa huotesha pembezoni mwa nyumba zao kwa kusudi la
kutumiwa kama kiungo cha chai, kinachojulikana kwa jina la lemongrass kwa lugha
ya kiingereza na cymbopogon kwa lugha za wataalam wa mimea, ilianza
kulimwa nchini uphilipino mnamo Karne ya 17 baadae ukaingia katika nchi
ya Haiti mwaka 1799 ambapo kilimo kilishamiri hadi mwaka 1917 wataalam wa
mimea wakaanzisha mashamba ya mchaichai kwa ajili ya utafiti Nchini marekani,
miaka ya 1947 soko la mchaichai ukarasimishwa katika jimbo la calfonia.
Mataifa mengine kama India, Sri lanka,
Argentina, Australia na kusini mwa Amerika kwa asilimia kubwa walitilia maanani
zao hilo hadi kufikia mwaka 1905 wataalam wa mimea kutoka sehemu mbalimbali
ulimwenguni walifanikiwa kuibua faida lukuki za mchaichai na kupelekea kuenea
dunia nzima.
Faida za mchachai kiafya.
Wataalamu wa mimea na lishe walithibitisha uwezo wa mchaichai kuwa inasaidia kutibu na kudhibiti magonjwa kama maumivu ya tumbo,maambukizi katika njia ya mkojo (U.T.I), inasaidia kusafisha figo na ini, matatizo ya moyo( Bp), inaimarisha utendaji kazi ya mishipa ya fahamu,inasaidia kudhibiti mlundikano wa mafuta katika mishipa ya damu (lehemu), inaondoa sumu mwilini, inaongeza kinga za mwili(CD4), inatibu Saratani, Inatibu kisukari aina ya pili,inatibu Baridi yabisi, Inaimarisha afya ya ngozi, inasaidia tatizo la kukosa usingizi (insomnia), inatibu maumivu ya tumbo la hedhi, inatoa gesi tumboni, inatibu homa za Mara kwa Mara, kutapika na maumivu ya viungo.
Wataalamu wa lishe na tiba kwa kutumia mimea na matunda, walibainisha kuwa uwezo huo ni kutokana na kwamba zao la mchaichai umesheheni virutubisho na misombo mbalimbali ambayo ni muhimu sana kwa afya ya binadamu kama vile
Vitamin A,B1 (thiamine ),B2(Riboflavin ),B3 (niacin ),B5 (pantothenic acid ),B6 (pyridoxine),folate na vitamin C pamoja na madini ya potassium, madini Chokaa, magnesium, manganese, Copper, zinc na phosphorus.
Mbali na virutubisho tajwa mchaichai ni zao pekee ambalo viambata tiba vinapatikana kwa kiasi kikubwa, ndio maana dunia inatizama kwa jicho la
tatu, kutokana na kemikali za aina yote.
Viambata tiba hivyo vinasaidia kudhibiti magonjwa hatarishi kama kupooza, aina mbalimbali za Saratani,vivimbe mwilini, matatizo ya mifupa na magonjwa sugu.
Hutibu shinikizo la juu la damu na unene kupita kiasi.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha wisconsin mwaka 1989, mchaichai una virutubisho vya madini ya potassium pamoja na misombo (compounds) za lemonal, citral na quercetin.
Aidha, utafiti uliofanyika December 2009 na kuchapishwa katka jarida la The Indian Journal of biochemistry and biophysics ulidhibitisha uwepo wa madini ya potassium, magnesium na misombo aina ya flavonoids katika mchaichai.
Wataalamu mbalimbali wanabainisha kuwa, virutubisho hivyo vinavyopatikana katika mchaichai vina uwezo mkubwa wa kuondoa mlundikano wa mafuta mwilini ambayo husababisha unene wa kupitiliza.
Pia huondoa mlundikano wa mafuta katika mishipa
ya damu, hivyo kuiruhusu damu
kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za miwili.
Kuondolewa kwa mafuta hayo katika mishapi ya damu
hushusha shinikizo la juu la damu na kufanya mapigo ya moyo kuwa
katika hali ya kawaida.
Sambamba na kudhibitiwa mlundikano wa lehemu
katika mishipa ya damu hasa ateri, huifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema,
pia na kinga dhidi ya ugonjwa wa kiharusi.
Jinsi ya kutumia.
Kupata tiba hiyo, majani ya mchaichai yalowekwe
katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani manne hadi
sita mgonjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai
kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni
kabla ya chakula cha jioni.
Mgonjwa anaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo
mno. Tafiti zinabainisha kuwa mtu mwenye Matatizo ya shinikizo la juu la
damu akitumia tiba hii kwa muda wa miezi miwili atakuwa
ameshaondokana na tatizo husika.
Tiba ya kisukari.
Wataalamu wa tiba kwa kutumia mimea na lishe
walibainisha kuwa katika zao la mchaichai una kirutubisho kinachofahamika kwa
jina la citral.Tafiti mbalimbali zinaelekeza kuwa,kirutubisho hicho huweka sawa
kiwango cha insulini mwilini.Hivyo kwa Wagonjwa wa Kisukari ambao kiwango chao
cha insulini ni kidogo,wanapotumia mchaichai wanapata faida kubwa kuudhibiti
ugonjwa wa kisukari .
Ifahamike kuwa,insulini ni kichocheo (hormone)
kinachotokewa na tezi ya kongosho ambacho kina kazi ya kuweka sawa kiwango cha
sukari mwilini. Wapo insulini itakuwa ndogo sana basi sukari itaongezeka na
kusababisha athari mbaya katika mifumo mbalimbali ya mwili.
Jinsi ya kutumia.
Kupata tiba hiyo,majani ya mchaichai huchemshwa
katika maji kisha maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai yatiwe unga wa
tangawizi kiasi cha vijiko 2 vidogo. Mgonjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe
1 asubuhi kabla kula kitu chochote na jioni kabla ya chakula cha usiku .Tiba
hii itumike kila kwa muda wa mwezi mmoja.
Hutibu vidonda vya tumbo
Pia huondoa mlundikano wa mafuta katika mishipa ya damu, hivyo kuiruhusu damu kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za miwili. Kuondolewa kwa mafuta hayo katika mishapi ya damu hushusha shinikizo la juu la damu na kufanya mapigo ya moyo kuwa katika hali ya kawaida.
Sambamba na kudhibitiwa mlundikano wa lehemu katika mishipa ya damu hasa ateri, huifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema, pia na kinga dhidi ya ugonjwa wa kiharusi.
Jinsi ya kutumia.
Kupata tiba hiyo, majani ya mchaichai yalowekwe katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani manne hadi sita mgonjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni kabla ya chakula cha jioni.
Mgonjwa anaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo mno. Tafiti zinabainisha kuwa mtu mwenye Matatizo ya shinikizo la juu la damu akitumia tiba hii kwa muda wa miezi miwili atakuwa ameshaondokana na tatizo husika.
Tiba ya kisukari.
Wataalamu wa tiba kwa kutumia mimea na lishe walibainisha kuwa katika zao la mchaichai una kirutubisho kinachofahamika kwa jina la citral.Tafiti mbalimbali zinaelekeza kuwa,kirutubisho hicho huweka sawa kiwango cha insulini mwilini.
Hivyo kwa Wagonjwa wa Kisukari ambao kiwango chao cha insulini ni kidogo,wanapotumia mchaichai wanapata faida kubwa kuudhibiti ugonjwa wa kisukari .Ifahamike kuwa,insulini ni kichocheo (hormone) kinachotokewa na tezi ya kongosho ambacho kina kazi ya kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini. Wapo insulini itakuwa ndogo sana basi sukari itaongezeka na kusababisha athari mbaya katika mifumo mbalimbali ya mwili.
Jinsi ya kutumia.
Kupata tiba hiyo,majani ya mchaichai huchemshwa katika maji kisha maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai yatiwe unga wa tangawizi kiasi cha vijiko 2 vidogo. Mgonjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe 1 asubuhi kabla kula kitu chochote na jioni kabla ya chakula cha usiku .Tiba hii itumike kila kwa muda wa mwezi mmoja.
Hutibu vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo
Chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo ni bacteria wanaofahamika kama Helicobacter pylori .Wataalamu wa lishe wanabainisha kuwa,kirutubisho cha citral kinachopatikana katika mchaichai kina uwezo mkubwa wa kuidhibiti bakteria hao hatari na hivyo kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
Jinsi ya kutumia.
Chemsha majani kumi za mchaichai Kwa maji kiasi cha nusu lita,mgonnjwa anywe maji hayo kiasi cha kikombe kimoja asubuhi na usiku kabla ya kulala.
Tatizo la maumivu makali wakati wa hedhi na kuvurugika mzunguko
Wataalamu
wa tiba kwa kutumia mimea tiba na lishe Walibaini kuwa,kunywa chai
iliyotengenezwa kwa kuchanganywa mchaichai na tangawizi ni tiba kwa
tatizo ya tatizo la maumivu makali ya tumbo yanayosababishwa na hedhi
pamoja na kurekebisha mzunguko wa hedhi uliovurugika.
Jinsi ya kutumia.
Kupata tiba hiyo,majani ya mchaichai huchemshwa
katika maji,kisha maji hayo kiasi kikombe cha chai yatiwe unga wa
tangawizi kiasi cha vijiko viwili vidogo,kisha mgonjwa anatakiwa kunywa
mchanganyiko huo vijiko vinne vikubwa Mara nne kwa siku kila baada ya masaa
matatu ndani ya siku saba hadi kumi na nne.
Husafisha figo

Unywaji
wa chai uliotengenezwa kwa mchaichai husaidia kuondoa sumu na takataka
mbalimbali mwilini.
Hii husaidia figo na Ini ambazo huusika na kazi
ya kuondoa sumu na taka mwili,hivyo ogani hizo huimarika pindi sumu na taka
mwili vikidhitiwa kwa kiwango cha juu hasa kwa kutumia lishe rafiki kama
mchaichai.
Jinsi ya kutumia
Wataalamu wa afya hushauri unywaji wa chai hiyo
japo kikombe kimoja asubuhi na jioni ili kupata faida hiyo.
Mbali na faida lukuki katka tasnia ya afya,
bidhaa zitokanazo na mchaichai zinazidi kuonekana kila leo sokoni.
Wakulima wa mchaichai hunufaika kwa
kiwango kikubwa ukilinganisha na mazao mengine, hekta moja inakadiriwa
kutoa lita Moja ya mafuta ya mchaichai ambayo dhamani yake ni milion saba
za kitanzania, mafuta hayo mbali na kutumika kutengenezea dawa za aina
mbalimbali kwa ajili ya binadamu ,pia inatumika kutengeneza sabuni,
manukato,mafuta ya kupaka na loshen.
NYONGEZA
Tafiti kadhaa zinaonesha kuwa mchaichai una
vichocheo muhimu vinavyoweza kupamban ana athari kadha wa kadha tumboni, kwenye
mkojo na hata kwenye vidonda.
Wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli