NA ZAINAB ATUPAE

FAINALI Coco Sport Ndondo Cup inatarajiwa kupifwa leo  katika uwanja wa Kiembe Samaki majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na gazeti hili Katibu wa Mashindano hayo Ali Makame,alisema fainali hiyo itapigwa kati ya Machicha na Team Prince.

Alisema baada ya kukosekana uwanja wa Amaan wamelazimika kutumia uwanja wa Kiembe Samaki licha ya kuwa ni mdogo.

“Tumeangalia viwanja vingi vya hapa Mjini,lakini tumekosa vyote ni vidogo hata viwanja vya Mao visinge tosha ndio tukaamua kutumia uwanja huu ambao tulianza na mashindano hayo na kumalizia fainali yetu,”alisema.

Aidha akizungumzia upande wa zawadi,alisema mshindi wa kwanza atapatiwa shilingi milioni 8,000,000 ,Kombe,Medali,Ngao pamoja na zawadi nyengine,huku mshindi wa pili atapata shilingi milioni 4,000,000,medali na zawadi nyengine.

Alisema zawadi nyengine zitakwenda kwa kocha bora,mchezaji bora, muamuzi bora,kipa bora pamoja na mshiriki bora.

Alisema sherehe mbali mbali zitakuwepo uwanja hapo pamoja na wasanii zenji flave kutoka visiwani Zanzibar  watatoa burudani.