NAIROBI, KENYA

MWENYEKITI wa kamati ya habari katika chama cha SPLM-IO cha nchini Sudan Kusini, Mabior Garang de’Mabior ametangaza kujiuzulu katika nafasi hiyo.

Mabior Garang de’Mabior, ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa zamani wa mambo ya ndani, alisema amejiuzulu nafasi hiyo akipinga hatua ya chama hicho kingie kwenye makubaliano ya amani.

“Naandika barua hii kukueleza kuwa nimejiuzulu nafasi ya kuwa mwenyekiti wa kaamti ya mawasiliano na msemaji wa chama cha SPLM-IO”, Garang de’Mabior aliwaeleza waandishi wa habari alichokiandika katika barua liyompelekea Riek Machar mkuu wa chama hicho.

Mabior alisema hawezi kufanyakazi na viongozi wa chama ambao sio wa kweli katika kusimamia makubaliano ya amani ambayo yatawahakikishia wananchi wa nchi hiyo wanaishi kwa amani.

Kujiuzulu kwa Mabior kumekuja kufuatia hapo awali kuwepo taarifa kwa atajiuzlu katika chama hicho kilichopambana kwenye vita na vikosi vya serikali ya Sudan Kusini.

“Tunapoingia kwenye makubaliano ya amani lazima yatekelezwe sio tunaingia kwa ajili ya kufurahisha watu bila kutekelezwa makubaliano ambayo yatawapa watu wa taifa hili amani ya kudumu”, alisema

Hata hivyo, viongozi waandamizi wa chama cha SPLM-IO, walikanusha kwamba Mabior anaweza kujiuzulu katika nafasi hiyo, ambapo hadi wakati huo alikuwa hajawasilisha barua ya kujiuzulu.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa Mabior amekuwa na tofauti kubwa baina yake na jenerali mwenye ushawishi mkubwa katika chama hicho

Lul Ruai Koang.