PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI, Olivier Giroud ambaye anakipiga na Chelsea amekuwa mfungaji bora wa pili kwa Ufaransa wakati wote, akimzidi Michel Platini kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ukraine ya ushindi wa 7-1.

Giroud (34), alifunga mara mbili katika kipindi cha kwanza na kufikisha idadi ya magoli 42 kwenye mechi yake ya 100 ya kimataifa, tisa yakiwa nyuma ya rekodi ya Thierry Henry.
Kijana Eduardo Camavinga (17), alifunga goli kwenye mechi yake ya kwanza na kuwa mfungaji wa pili mdogo wa Ufaransa.

Kiungo, Corentin Tolisso, Kylian Mbappe na Antoine Griezmann wote walicheka na nyavu.
Kikosi cha Didier Deschamps pia kilifaidika na bao la kujifunga la Vitaliy Mykolenko na ingawa Viktor Tsygankov alifunga na kuweka matokeo 4-1, wageni walizidiwa jijini Paris.

Ushini huo uliashiria kipigo kibaya zaidi katika historia ya Ukraine, na timu hiyo sasa inasimamiwa na mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Chelsea, Andriy Shevchenko.(AFP).