NAIROBI, Kenya

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Kenya Gor Mahia wameachana na kocha Steven Polack kwa makubaliano ya pande zote.

 Polack aliandika barua kwa klabu akielezea kwamba kuporomoka kwa uchumi kumeathiri sana timu na biashara kote ulimwenguni na ndio sababu yake ya kuamua kuondoka.

“Klabu na mimi tumefika makubaliano ya pamoja kumaliza mkataba wangu kutokana na mtikisiko wa uchumi na janga la corona ambalo haliathiri Gor Mahia tu, bali pia klabu nyingine na wafanyabiashara kote ulimwenguni,” ilisema barua ya Polack.