PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI wa FC Barcelona, Antoine Griezmann, ameendelea kuwa sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wanaowania kuifika na kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote.
Rekodi hiyo katika timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa inashikwa na aliyewahi kuwa mshambuliaji na nahodha wake, Thierry Henry, aliyepachika mabao 51.

Griezmann anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaodhamiria kuifikia na kuivunja rekodi hiyo, baada ya kufunga dhidi ya Croatia, huku mwishoni mwa wiki iliyopita akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Ujerumani.
Idadi hiyo imekuja baada ya juzi kufunga bao la kwanza kwa Ufaransa dakika ya nane ya mchezo akilisaidia taifa lake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia huku Croatia wakitawala zaidi kipindi cha pili na kuwezesha kusawazisha kunako dakika ya 64 kupitia kwa Nikola Vlasic, lakini, harakati hizo hazikuzaa matunda kwani Ufaransa walirudi na kufunga bao la ushindi kupitia kwa Kylian Mbappe.

Mbappe sasa ameifungia Ufaransa mabao 16 na kumfanya awe sawa na Franck Ribery na Laurent Blanc, huku Griezmann akiwa nyuma kwa goli moja, akitanguliwa na mshambuliaji wa zamani wa ‘Les Bleus’, David Trezeguet.
Wafungaji Bora wa timu ya taifa ya Ufaransa wakati wote ni Thierry Henry (51), Olivier Giroud (42), Michel Platini (41), David Trezeguet (34) na Antoine Griezmann (33).

Wakati huo huo, wachezaji wa wote wa Juventus wamelazimika kujitenga kwa ridhaa yao baada ya kiungo wa timu hiyo, Weston McKennie kuthibitika kuwa na virusi vya ‘corona’.

McKennie ambaye amejiunga na Juventus katika dirisha hili la usajili akitokea Schalke ya Ujerumani.
Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni saa kadhaa zimepita tokea Cristiano Ronaldo athibitike pia kuwa na maambukizi ya ‘corona’ akiwa kwao Ureno na sasa amejitenga.(AFP).