NA MWANAJUMA ABDI, DAR ES SALAAM

GAVANA wa Benki Kuu Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga, amesema maombi ya usajili au ya leseni kwa watoa huduma ndogo za fedha yamesongezwa mbele hadi Aprili 30, mwakani.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, amesema BOT imepokea maombi ya wadau wengi ya kuongeza muda wa usajili na utoaji lesseni, ili waweze kuwasilisha maombi yanayoendana na matakwa ya sheria na kanuni husika.

Alisema kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, anapenda kuutaarifu umma kuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya usajili au ya leseni yamesogezwa hadi Aprili 30, 2021.

Alieleza anatarajia muda huo ulioongezwa utawawezesha watoa huduma ndogo za fedha katika madaraja yote kufanya maandalizi ya kutosha na kuwasilisha maombi yaliyokamilika na yanayokidhi matakwa ya sheria na kanuni.

“Mnamo mwezi Disemba 2019, BOT ilitoa taarifa kwa umma kuhusu sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 iliyoanza kutumika rasmi Novemba 1, 2019”, alisema.

Alifafanua taarifa hiyo ilirejea kifungu cha 57 cha sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, ambacho kinawataka watoa huduma ndogo za fedha wote kuwasilisha maombi ya leseni au usajili Benki Kuu ya Tanzania au kwenye Mamlaka kasimishwa katika kipindi cha miezi 12 baada ya sheria kuanza kutumika Oktoba 31 mwaka huu. Prof. Florens, alisema watoa huduma ndogo za fedha walio