KABUL, AFGHANISTAN

AJALI ya ndege mbili za kijeshi aina ya helkopta za Afghanistan zimesababisha wanajeshi kujeruhiwa huko kusini mwa jimbo la Helmand na wengine tisa kufariki.

Kwa mujibu wa maofisa walisema, tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano katika kitongoji cha Nawa, ambapo ajali hiyo ilisababishwa na tatizo la kiufundi, na kupelekea waliokuwemo ndani ya ndege hizo wote kufariki.

Hivi karibuni eneo hilo limekuwa na mapigano kati ya Taliban na jeshi la serikali ya Afghanistan, wakiungwa mkono na wanajeshi wa angani kutoka Marekani.

Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea pembezoni mwa mji wa Lashkar Gah, ambako kulikuwa tayari kumedhibitiwa.

Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu 35,000 wamelazimika kuhama makazi yao huko Helmand.

Hili ni shambulio kubwa zaidi la Taliban kutokea na kuchukua muda mrefu, ambapo mwezi uliopita majadiliano ya amani yalianza.