HORMUZ ni eneo jembamba ambalo hutumika kama mlango wa kuzifikia nchi kadhaa za mashariki ya kati kupitia ghuba ya bahari ya Oman.
Unapotaka kusafiri kwa kutumia bahari na unahitaji kuzifikia nchi za Iran, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Bahrain, Iran, Saudi Arabia na Kuwait, lazima upitia kwenye mlango wa Hormuz.
Hormuz limekuwa moja ya eneo muhimu kwa uchumi wa dunia, kwani mkondo huo wa bahari ndio njia kuu inayotumiwa na meli katika eneo la ghuba hasa kwa ajili ya usafirishaji wa nishati ya mafuta.
Licha ya udogo wake, mkondo wa bahari wa Hormuz ndio njia muhimu zaidi duniani inayopitia meli kubwa zinazosafirisha mafuta kutoka nchi za mashariki ya kati kuelekea maeneo mbalimbali duniani.
Eeno hilo lina una urefu wa maili 96 na upana wa maili 21 katika eneo lake jembamba huku kukiwa na njia mbili za meli katika pande zote mbili zenye upana wa maili mbili.
Huku ukipakana na Iran upande wa kaskazini na Oman upande wa Kusini pamoja na UAE, mkondo wa Hormuz unaunganisha eneo la ghuba na bahari ya Uarabuni.
Mkondo huo una kina kirefu kwa meli kubwa za mafuta na hutumika na wazalishaji wa gesi mashariki ya kati pamoja na wateja wao.
Kila wakati kuna meli kadhaa za mafuta zinazoelekea katika mkondo wa Hormuz ama kutoka zikiwa inakwenda kubeba mafuta ama zimeshabeba mafuta na kuelekea sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Je ni kiwango gani cha mafuta kinachopitia eneo hilo?
Kwa mujibu wa taarifa mlango wa Hormuz unapitisha robo tatu ya gesi inatumika katika mataifa mbalimbali ulimwenguni na pia mlango huo unapitisha asilimia 25 jumla ya mafuta yanayotumika ulimwenguni.
Takriban mapipa milioni 21 ya mafuta kwa siku yanapitisha kwa meli kupitia mkondo wa Hormuz, hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019.
Mnamo mwaka 2016, mwaka ambao takwimu zinaweza kupatikana, mkondo huo ndio uliokuwa na biashara nyingi za mafuta duniani kuliko sehemu nyengine yoyote.
Ulibeba takriban mapipa milioni 19 ya mafuta kwa siku, zaidi ya milioni 16 kwa siku ambayo yalipitia mkondo wa bahari wa Malaca, njia muhimu ya kimataifa katika bahari hindi.
Ukilinganisha na mapipa milioni sita kwa siku yaliopitia kupitia mfereji wa Suez Canal Bab el-Mandeb katika bahari nyekundu.
Mkondo wa bahari wa Hormuz ni muhimu kwa wauzaji wa mafuta katika eneo na nchi za ghuba, ambalo uchumi wake unategemea uzalishaji wa mafuta na gesi.
Mwaka 2018, Saudia iliuza takriban mapipa milioni 6.4 ya mafuta kila siku na biashara yake hiyo ulipitishwa kupitia mkondo huo kuelekea katika matifa mbaimbali ulimwneguni.
Aidha Iraq katika mwaka huo huo, ilisafirisha nje ya nchi hiyo mapipa milioni 3.4, UAE mapipa milioni 2.7 na Kuwait mapipa milioni mbili yote hayo yalipitishwa katika ukanda huo.
Iran pia hutegemea sana njia hii kwa uuzaji wa mafuta ughaibuni, Qatar, ambalo ndio taifa kubwa linalozalisha gesi ya maji, huuza gesi yake kupitia mkondo huo.
Mkondo huo umekuwa muhimu katika miaka ya hivi karibuni kwa mataifa yenye uchumi mkubwa barani Asia.
Kiwango kikubwa cha mafuta kinachopitia mkondo huo wa bahari 2018 kilienda nchini China, Japan, Korea Kusini na India. Marekani pia iliagiza mapipa milioni 1.4 kwa siku kupitia njia hiyo.
Uingereza huagiza mafuta kutoka ghuba kupitia mkondo wa Hormuz pamoja na thuluthi moja ya gesi kwa ajili ya matumizi hupita katika eneo hilo.

Je kuna njia nyengine za kupitishia mafuta?
Mkondo wa bahari wa Hormuz bado ndio njia bora ya kusafirisha kiwango kikubwa cha mafuta kutoka eneo la ghuba na njia pekee kupitia baharini.
Kuna njia za ardhini ambazo pia hutumika kusafirisha mafuta kutoka eneo la Ghuba.
Bomba la mafuta la Saudia linaelekea katika bahari nyekundu, na lina kiwango cha mapipa milioni tano ya mafuta kwa siku.
Abu Dhabi nayo ina bomba la mafuta ambalo hubeba takriban mapipa milioni 1.5 ya mafuta kwa siku katika pwani yake na kusafirisha mbele ya mkondo wa Hormuz.
Na kuna bomba jengine la mafuta linaloweza kusafirisha mafuta ya Iraq hadi pwani ya Mediterenean, lakini sio kwamba mabomba haya ya mafuta yanafanya kazi asilimia 100.
Aidha mabomba hayo hayawezi kusafirisha kiwango kikubwa cha mafuta kama kile kinachosafirishwa na meli zinazopita katika eneo la Hormuz.
Je Iran inadhibiti mkondo wa bahari wa Hormuz?
Sheria za Umoja wa mataifa zinaruhusu mataifa yote kudhibiti maili 13.8 kutoka kwa pwani yake. Hiyo inamaanisha kwamba eneo jembamba zaidi la mkondo huo lipo kati ya Iran na Oman.
Iran huruhusiwa kuendeleza shughuli zake katika maji yake, lakini sio kuathiri safari za meli nyengine za kigeni. Marekani sasa imeimarisha uwepo wa jeshi lake katika eneo hilo.
Lakini imesema kuwa ni vyema kwa mataifa mengine kufanya juhudi za kuimarisha usalama katika eneo la Ghuba na eneo zima kwa jumla. Na Uingereza imetoa meli ambazo zitaweka usalama katika mkondo wa Hormuz.