YEREVAN,ARMENIA

WIZARA ya Ulinzi ya eneo la Nagorno-Karabakh imesema kwamba wanajeshi wake 51 wameuawa na kuifanya idadi jumla ya vifo kufika 1,119 tangu kuanza mapigano mnamo Septemba 27 kati ya Azerbaijan na Armenia.

Mapigano yamezidi kuwa mabaya tangu miaka ya 1990, wakati ambapo karibu watu 30,000 waliuawa.

Yanatajwa kuwa ni mapigano mabaya zaidi kwa karibu miaka 30, ambayo yaliongeza hofu ya vita kupanuka na kuzijumuisha Urusi na Uturuki ambayo ni mshirika wa Azerbaijan.

Mapigano hayo pia ni tishio kwa mabomba yanayobeba mafuta na gesi kutoka Azerbaijan na kuyasambaza kote ulimwenguni.

Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu ilisema pande zote mbili ziliangusha makombora katika maeneo ya mijini.