WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibarleo, leo hii nimewatayarishi tiba asilia kwa kutumia mti wa Alovera (Mshubiri). Kwa hakika mti licha ya uchungu wake lakini hutibu maradhi lukukji ya binaadamu kiasi kwamba watu wengi huusafiria mti huu.

Kama una moja ya matatizo yafuatayo basi tumia mti huu nawe utaona faida yake.

FAIDA 30 ZA MMEA WA ALOE VERA AU MSHUBIRI

1. Huondoa uvimbe katika jicho

Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe.

2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito

Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.

3. Hutibu bawasiri

Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri. Chana tawi la aloe vera freshi na upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi hapo uvimbe huo utakapopotea.

4. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo

Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya tumbo kama kuum, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.

5. Huziimarisha kucha dhaifu

Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.

6. Huondoa Mikunjo ya uso

Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.

7. Husafisha ngozi na kuondoa alama zitokanazo na kuungua na jua

Chunusi, ukurutu na kuungua kwa ngozi kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe-vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone umepona kabisa. Mu-aloe vera pia una sifa ya kupoza kama ilivyo menthol ambayo unaufanya Mu-aloe vera kuwa dawa ya asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.

8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya kunyoa

Aloe Vera ni dawa ya asili katika kutibu michubuko asante kwa vimeng’enya vyake ambavyo huwa na kiasi kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu pakaa jeli ya aloe vera na hata baada ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo na kunyoa.

9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi

Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.

Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.

10. Hutibu homa na mafua

Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine mhimu.

11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama (Vegans)

Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.

12. Huongeza nguvu mwilini

Matumizi mengine ya kitabibu ya mmea wa mu aloe vera au mshubiri kwa kiswahili chake hasa, ni kuongeza usawa wa nguvu mwilini. Hii ni kutokana na uwepo wa vitamin b 14 na viinilishe vingine ambavyo husaidia kubadili asilimia kubwa ya chakula katika tumbo lako na kuunda nguvu.

13. Huondoa mba kichwani

Changanya jeli ya asili ya aloe vera na shampoo yako, dakika chache kabla ya kwenda kulala pakaa vizuri mchanganyiko huo kwenye nywele zako na uache zikauke kidogo na usafishe nywele zako asubuhi.

14. Huondoa maumivu wakati wa hedhi

Changanya jeli ya Aloe vera na pilipili manga ya unga kidooogo, meza kijiko cha chakula kimoja mara tatu kwa siku kila siku hadi maumivu yatakapoacha.

15. Hulainisha nywele

Jeli ya Aloe vera ni nzuri katika kutibu tatizo la nywele kujisokota na ni mbadala mzuri kwa bidhaa nyingi za madukani zenye gharama kwa ajili ya nywele.

16. Ni dawa ya asili ya kusafishia mdomo

Changanya jeli ya aloe-vera ml 100, vijiko 3 vya chai vya baking soda, maji ml 100 na kijiko 1 kidogo cha juisi ya limao. Changanya vizuri vyote kwa pamoja na utumie kama dawa yako ya asili ya kusafishia mdomo.

17. Hutibu matatizo katika mmeng’enyo wa chakula

Juisi ya Aloe vera ni nzuri sana katika kurekebisha matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, hurekebisha kuvurugika kwa tumbo na kiungulia. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.

18. Hushusha lehemu (Cholesterol)

Tafiti zimeonyesha kuwa kunywa juisi ya aloe vera kwa kipindi kirefu kunaweza kushusha kiwango cha lehemu mwilini. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.

19. Hutibu chunusi

Aloe Vera huondoa chunusi kwa kuziondoa seli zilizokufa katika ngozi na hivyo kuvifungua vishimo katika ngozi na kuondoa mafuta yaliyoganda katika hivyo vishimo. Pakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja katika eneo lililoathirika na chunusi. Pia makovu yaliyoachwa kutokana na chunusi yanaweza kuondolewa kwa kupakaa jeli ya aloe vera pekee.

20. Hutibu ukurutu na upele

Ukurutu ambao ni matokeo ya juu ya tetekuwanga kwa kawaida hutokea kwa watu wazima wenye kinga ya mwili pungufu. Aloe Vera inaweza kutumika kutibu tetekuwanga zinazosababishwa na kirusi aina ya herpes virus. Kwa kupakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja kwenye sehemu zilizowazi hutanua mishipa ya damu jambo linalosaidia kutibu vidonda.

21. Huzuia ngozi kuunguzwa na jua (Sunscreen)

Kupakaa jeli ya Aloe Vera katika mwili hulinda ngozi dhidi ya miale yote ya jua kutua moja kwa moja kwenye ngozi na hivyo kukufanya usizeeke mapema, pia ni dawa nzuri kwa ngozi inayofubaa.

22. Hulainisha sehemu kavu za siri

Aloe Vera hufanya kazi kama kilainishi bora kabisa cha asili katika maeneo ya siri kwa jinsia zote mbili na kutoa unyevunyevu wa asili.

23. Hutibu vidonda katika mdomo

Mu Aloe vera unazo vitamini na asidi amino ambazo husaidia kuzitengeneza upya tishu zilizoharibika. Tafiti zimeonyesha kuwa watu wanaosumbuliwa na vidonda mdomoni waliotumia jeli ya aloe vera walifanikiwa kutibu karibu asilimia 50 haraka zaidi kuliko wale ambao hawakutumia jeli ya aloe vera.

24. Hutibu maambukizi katika uke

Unaweza kutibu maambukizi katika uke kwa kupakaa jeli ya aloe vera kwa nje na kwa kuinywa jeli kupata faida yake ya kutibu fangasi. Mililita 120 mpaka 200 za jeli ya aloe vera kila siku zinaweza kusaidia kutibu maambukizi na fangasi katika mwili na ikiwa utaendelea kuinywa kwa muda mrefu kunaweza kuzuia maambukizi zaidi kutokujirudia baadaye.

25. Husaidia wawindaji

Wawindaji wa wanyama katika barani Afrika mara kwa mara hupakaa jeli ya aloe vera katika miili ili kupunguza kutokwa jasho na kuondoa harufu yao ya asili katika mwili isisikike na wanyama.

26. Suluhisho kwa watafuna kucha

Burashi kucha za mtoto anayependa kutafuna kucha na jeli ya aloe vera, ile ladha ya uchungu katika aloe vera kutamfanya aache kuzitafuna kucha zake.

27. Hutumika katika kupunguza uzito

Watafiti wameweza kugundua kuwa kunywa juisi ya aloe vera husaidia kupunguza sukari kwenye damu jambo mhimu kwa wale wenye kisukari cha aina ya pili. Wanasayansi wanaamini kuwa kuweka kiwango cha sukari chini hupunguza uzito.

28. Hutibu upungufu wa damu (Anemia)

Kunywa jeli ya aloe vera kunasaidia uzalishaji zaidi wa seli nyekundu za damu katika mwili wako na hivyo kutibu tatizo la kupungua kwa damu.

29. Huondoa maumivu ya mishipa

Kutokana na sifa yake ya kutibu uvimbe, unaweza kutibu uvimbechungu (inflammation) katika maungio yanayopelekea maumivu katika mishipa kwa kupakaa jeli ya aloe vera katika eneo unalosikia maumivu.

30. Hutibu maumivu katika sikio

Matone kadhaa ya aloe vera yakinyunyizwa sikioni yanaweza kuleta nafuu kubwa kama unapatwa na maumivu katika masikio. Hii ni nzuri pia kwa masikio yanayotoa usaha na maumivu mengine katika masikio.