Yamfungia siku tano kutofanya kampeni

NA KHAMISUU ABDALLAH

KAMATI ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imemsimamisha mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif sharif Hamad kufanya mikutano ya kampeni.

Kusimamisha huko kumeanza rasmi leo hadi Oktoba 20 mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya uvunjifu wa maadili, adhabu ambayo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 23 (d) cha kanuni za maadili ya uchaguzi mwaka 2020.

Mwanasheria wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambae pia ni Katibu wa Kamati ya maadili Khamis Issa Khamis alieleza hayo jana wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya uamuzi wa kamati ya maadili dhidi ya Ameir Hassan Ameir aliyemlalamikia mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Alisema uamuzi huo unatokana na kamati hiyo kusikiliza lalamiko la mgombea urais wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir dhidi ya mgombea huyo katika mkutano wake wa Oktoba 13 uliofanyika katika kiwanja cha Jadida Wete Pemba.

Maalim Seif alitoa kauli ya kuhamasisha wanachama wake kwenda katika vituo vya kupigia kura Oktoba 27 kinyume na kifungu cha 82(1) (2) cha sheria ya uchaguzi ambacho kimewataja watu maalum.

Alisema kifungu hicho kimewataja watu maalum wakiwemo watendaji wa uchaguzi na wapiga kura wanaohusika na ulinzi siku ya uchaguzi ambao wanaohusika na ulinzi siku hiyo ambao wanahusika na upigaji wa kura ya mapema.

Hata hivyo, alisema haki ya rufaa imetolewa kwa mgombea huyo ikiwa hakuridhika na uamuzi wa kamati hiyo. Kaamti hiyo ilikaa jana katika kituo cha ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maruhubi chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Jaji Khami