NA MWANAJUMA MMANGA

MENEJA  wa Kampuni ya Faki Rice, Yussuf Faki Yussuf, amesema anatarajia kupata mpunga mwingi kutoka kwa wakulima mara hii kushajiika kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko Kaskazini, ambapo alisema serikali imejipanga kuhakikisha kuboresha miundombinu ya kisasa mbali mbali ya zao la mpunga kwa wakulima.

Aidha, alisema serikali imekuwa ikiboresha maeneo ya kilimo pamoja na kuwapatia pembejeo, elimu, Mabibi, na mabwanashamba, ili kuongeza uzalishaji wa zao hili na kuleta tija zaidi.

Hivyo amewataka wakulima kuwa na ari ya kujituma kulima zaidi zao hilo kwa kutumia taaluma waliyoaptiwa na kutumia miongo ya hali ya hewa,  ili kuweza kupata mavuno mengi.

‘Mwaka huu sikuweza kupata mpunga mwingi kutokana na kuathirika kwa maradhi ikiwemo kuvamiwa na wadudu pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri mpunga huo” alisema.

Alisema mara nyingi mpunga wake huwa ananunua kwa wakulima ambapo mara hii  matarajio yake kununua tani 100 za mpunga kwa wakulima  wenye thamani ya shilingi Milioni 80 kwa msimu ujao mwakani, na tayatari ameshanunua  jumla ya tani 26 za mpunga kupitia wakulima hao kwa msimu wa mwaka huu, na anatarajia kuzalisha tani 31 mwaka huu.