TOKYO,JAPAN

KAMPUNI tatu za Japani zinaungana kutengeneza meli za mafuta zinazotumia umeme kikamilifu bila matumizi ya kaboni hata kidogo.

Ushirikiano huo ni kati ya kampuni mbili za kutengeneza meli, na kampuni ya kutengeneza mashine ya Kawasaki Heavy Industries.

Kampuni hizo mbili za kutengeneza meli zitatengeneza meli mbili kila moja ikiwa na urefu wa mita 60 na uzito wa tani 499.

Kampuni ya Kawasaki itatoa betri za lithium-ion za kuendesha meli hizo.Utengenezaji wa meli hizo unatarajiwa kukamilika Machi mwaka 2022.

Zitagharimu fedha nyingi kuzitengeneza kuliko meli za kawaida zinazotumia mafuta mengi, lakini zitahitaji wafanyakazi wachache kuziendesha, ikiwa ni manufaa makubwa kwa sekta hiyo inayokabiliwa na uhaba wa wafanyakazi.