NAIROBI, Kenya
BINGWA wa mbio za nyika nchini Kenya, Kibiwott Kandie, amesisitiza, analenga kumzidi ujanja mfalme wa dunia katika mbio za mita 5,000, Joshua Cheptegei ambaye ni raia wa Uganda, kwenye nusu marathoni ya dunia itakayofanyika Gydnia, Poland Oktoba 17.

Ingawa nguli wa riadha raia wa Ethiopia, Haile Gebreselassie, anampigia upatu Cheptegei kutamba katika mbio hizo za Poland, Kandie amesisitiza kwamba hana sababu yoyote ya kuhofia.

Kandie atalenga kuendeleza matokeo ya kuridhisha yaliyomshuhudia akiibuka mshindi wa RunCzech Half Marathon jijini Prague katika Jamhuri ya Czech Septemba 2020 kwa kutumia dakika 58:38 kwenye kivumbi hicho.(AFP).