NA MARYAM HASSAN

KIJANA aliyedaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kete 118 amefikishwa katika mahakama ya mkoa Mwera kujibu tuhuma hizo.

Kijana huyo ni Ibrahim Jumanne Kara (23) mkaazi wa Tunguu amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Khamis Ali Simai.

Akisoma Shtaka wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Shumbana Mbwana, alidai kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 13, mwaka huu majira ya saa 9:00 za jioni huko Jumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.

Mshitakiwa alipatikana akisafirisha kete hizo zikiwa ni unga unaosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya aina Heroin zenye uzito wa gramu 2.369 jambo ambalo ni kosa kisheria.

 Alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (a)(i) cha sheria nambari 9 ya mwaka 2009, kama ilivyorekebiswa na kifungu cha 23 cha sheria nambari 1 ya mwaka 2019 sheria ya Zanzibar.

Mara baada ya kusomewa shitaka lake mshitakiwa huyo alikataa na kuiomba mahakama kumpa dhamana, jambo ambalo lilipingwa kwa madai kuwa kiwango alichopatika nacho ni kikumbwa.

Baada ya kutoa pingamizi hizo aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo na kupangwa tarehe nyengine kwa ajili ya kusikilizwa ushahidi jambo ambalo lilikubaliwa.