KATIKA kipindi cha miaka iliyopita, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yo-jong ameonekana kama mtu muhimu katika uongozi wa Pyongyang.

Yo-jong ni dadake mdogo kiongozi mkuu wa taifa hilo Kim Jong-un na dadake wa pekee anayeonekana kuwa karibu na uongozi na mwenye uwezo mkubwa.

Ni binti mdogo wa hayati Kim Jong-il. Ni ndugu wa mama na baba wa Kim Jong-un na Kim Jong-chol, kaka yake ambaye hakuwahi kudhaniwa kuwa ni kiongozi wa juu katika mfumo wa uongozi wa kisiasa.

Kim Jong-chol,

Inaaminika alizaliwa mwaka 1987, ni mdogo kwa miaka minne wa kaka yake Kim Jong-un. Ndugu hao wawili walisoma na kuishi pamoja huko Berne, Switzerland.

Maofisa wa skuli nchini Switzerland wamesema alilindwa zaidi na kitengo cha walinzi na walezi, ambapo wakati mwingine aliripotiwa kuwa na homa kali na alitolewa skuli na kupelekwa hospitalini.

Kutoka mwaka 2014, kazi yake kubwa ilikuwa ni kuilinda taswira ya kaka yake, alikuwa na jukumu muhimu kwenye chama hususan kwenye idara ya propaganda.

Kabla ya mwaka 2014 mwanamke huyo alikuwa akionekana mara chache sana kwenye vyombo vya habari, mwaka 2011 alionekana kwenye msiba wa Baba yake pamoja na kwenye uchaguzi wa kaka yake mwaka 2014.

Mnamo mwaka 2017 alipandishwa hadhi, hii ikaonekana kuwa amepata nafasi kubwa ijapokuwa majukumu yake ya propaganda yalibakia palepale.

Alidaiwa kusimamia matukio yote ya kaka yake yaliokuwa yakihusu kuonana na jamii pamoja na kuwa mshauri wa kisiasa.

Yo-jongkwa mara ya kwanza alijipatia umaarufu wa kimataifa 2018, wakati alipokuwa ndugu wa kwanza wa familia ya Kim kuzuru Korea Kusini.

Dada huyo alikuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliokuwa yakifanyika mjini Seoul ambapo Korea Kuisni na Korea Kaskazini zilishindana kama timu moja.

Hatua hiyo ya mwaka 2018 ambapo alifanyakazi ya kidiplomasia pamoja na nduguye ilimfanya akutanea na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae – in, Xi Jingpin wa China na rais wa Marekani Donald Trump.

Uhusiano wa karibu na nduguye na majukumu yake makubwa katika ngazi za kisiasa yamemfanya kuangaziwa tena mwezi Aprili 2020 katika kipindi ambapo Kim Jong un alitoweka katika hafla za umma.

Wakati Kim alipotoweka mwezi Aprili mwaka huu, maswali mengi kuhusu afya yake yalizuka, ambapo miongoni mwa watu waliokuwa wakidhaniwa kuwa atachukua nafasi ya uongozi endapo Kim Jong-un atafariki ni dada yake huyo.

Jukumu la Yo-jonglilipigwa jeki mnamo mwezi Oktoba mwaka 2017 wakati alipopandishwa cheo hadi katika kamati kuu ya kisiasa ya chama tawala nchini humo.

Kabla ya hilo Yo-jongalikuwa naibu mkurugenzi wa idara ya propaganda- jukumu ambalo anaendelea kulibeba na mara nyingi anafanyia kazi muonekano wa kama kiongozi wa juu nchini humo.

Yo-jong pia amewekwa katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo kufuatia madai kwamba anahusika na unyanyasaji wa kibinadamu nchini Korea Kaskazini.

Kutokana na vikwazo alivyoekewa dada huyo inamaanisha kwamba raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara yoyote naye na mali yake yoyote iliopo nchini Marekani itapigwa tanji.

Wakati wa mkutano mkuu wa Hanoi 2019 uliposhindwa kufikia makubaliano na Marekani, ilidhaniwa kuwa huenda angeshushwa katika wadhifa wa juu wa kisiasa, lakini mwanzoni mwa mwaka 2020 akarejea.

Je Yo-Jong ana uwezo kiasi gani?

Ni vigumu kuelewa uwezo wake nchini Korea Kaskazini, hivyo basi ni vigumu kubaini mtandao wake wa kisiasa hata hivyo zipo taarifa kwamba ameolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala mwenye uwezo mkubwa na mtu wa pili kwa uwezo baada ya rais Kim Jong-un.

Hivi karibuni, taifa hilo lilihusika kutuma ujumbe wa maneno makali dhidi ya Korea Kusini na kuonekana kama ni namna mpya ya Korea Kaskazini kuingilia masuala ya Korea Kusini.

Mnamo mwezi Juni mwaka huu, Yo-jong alitishia kutuma kikosi cha wanajeshi katika ukanda wa mpakani, ikiwa ni sehemu ya kile ambacho Pyongyang ilisema walishindwa kuzuia wanaharakati wanaopinga utawala wake kutuma vijibarua vinavyopinga uongozi wake.

Mwanamke huyo alitoa angalizo pia kuwa ofisi zote ambazo zina uhusiano kati ya nchi hizo mbili na ziko eneo la mpakani katika mji wa Kaesong ambako Korea Kaskazini ilijitoa tangu Machi 2019, zitaondolewa.

Siku chache baadae mnamo Juni 16 mwaka huu, mlipuko mkubwa ulisikika huko Kaesong na moshi ulionekana ukifuka katika eneo hilo, ambapo maofisa wa Seoul walithibitisha kuwa ofisi ambayo serikali ya Korea Kusini ilitoa karibu dola milioni 8 ili kufanyiwa ukarabati ndio iliyoripuliwa.

Siasa za nchi hiyo kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiogopa ukoo ambao unafahamika kama Paektu kurejea katika utawala wa mwasisi wa taifa hilo Kim Il-sung.

Ilhali Kim ni miongoni mwa wanafamilia hiyo, hivyo chombo cha habari cha taifa kinabidi kipate namna ya rahisi ya kutoa madaraka katika mikono yake.

Lakini kama ni familia hiyo ina maanisha kuwa alikuwa hajachaguliwa na kiongozi mpya anaweza kumuona kama mpinzani wake ambaye ni hatari kwake.

“Labda kama mwanafamilia mwingine wa Kim atachukua majukumu hayo, basi kwake mambo yatakuwa ni rahisi sana,” alisema Fyodor Tertitskiy kutoka chuo kikuu cha of Kookmin Korea Kusini.

“Au kukubali kuchukua uongozi huo wa juu au kupoteza madaraka yote na kuharibu maisha yake pia.”

Hata hivyo, jukumu lake kama mrithi wa kaka yake limekuwa likizungumzwa kila wakati kunapokuwa na wasi wasi wa kiafya wa Kim Jong-un.