LONDON, England

JURGEN Klopp, kocha Mkuu wa Liverpool amesema hataki kuamini kwamba wamepoteza mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu England kwa kupokea kichapo cha mabao 7- mbele ya Aston Villa.

Usiku wa kuamkia jana Oktoba 5, Liverpool ilikuwa ndani ya Uwanja wa Aston Villa Park kusaka pointi tatu muhimu na kuambulia kichapo cha mabao 7-2 jambo lililomfanya Klopp asiamini anachokiona.

Mabao ya Aston Villa yalifungwa na Ollie Watkins dakika ya 4,23 na 39 na kumfanya asepe na mpira wake, John McGinn dk 35, Ross Barkley dk 55 na Jack Grealish alitupia mawili dakika ya 66 na 75.

Huku yale ya Liverpool yakifungwa na Mohamed Salah dakika ya 33 na 65.

Klopp amesema:”Ulikuwa ni usiku mbaya kwetu na wachezaji pia, sitaki  kuamini kwamba tumefungwa mabao mengi ila kwa kuwa imetokea hamna namna acha kuangalia tutafanyaje mechi zijazo.

“Hatukupaswa kufungwa kwani tulikuwa tunatengeneza nafasi pia tena nyingi ila mambo hayakuwa mazuri kwetu hii ni mbaya hatupaswi kukata tamaa.”