NA ZAINAB ATUPAE

 MABAHARIA wa KMKM  inayoshriki ligi kuu Zanzibar imeondoka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Uhamiaji inayoshiriki ligi daraja la kwanza kanda ya Unguja, katika muendelezo wa michezo wa kirafiki.

Mchezo huo ulipigwa juzi huko uwanja wa Mchangani Shamba majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo huo uliokuwa wa ushindani ambapo KMKM ilitawala mchezo muda mwingi.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko KMKM ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, ambayo yote yalifungwa na mshambuliaji  Mateo Antoni  katika dakika ya  10 na 25 na  kudumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili timu hizo zilingia na mabadiliko makubwa,huku kila timu ikisaka mabao kwa mwenzake,lakini dakika ya 65 Mateo Antoni tena alipachika bao la tatu.

Bao la nne lilifungwa na Iliyasa Suleiman dakika ya  70,huku bao la tano lilimaliziwa na Mohamed Mesi dakika ya 84.

 Bao la kufutia macho la timu ya Uhamiaji lilifungwa na Suleiman Mpote dakika ya 88.