NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KOCHA wa KMC Habibu Kondo amesema ushindi wa Yanga wa mabao 2-1 dhidi ya timu yake umechangiwa na waamuzi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara KMC akiwa mwenyeji ulichezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana kwa njia ya simu, Kondo alisema Yeye ameona kikosi chake kimecheza vizuri na kilikuwa na ari ya kupata ushindi lakini waamuzi waliwavuruga.

Alisema wapinzani wao wamepata ushindi ambao anahisi wamesaidiwa na waamuzi kinyume na hivyo Yanga isingeweza kushinda.

Kocha Habibu alisema kila mtu aliyeangalia mchezo aliona jnisi gani waamuzi walivyochezesha mchezo huo kwa upendeleo, jamboa ,mbalo lilimesaidia Yanga kupata kupata ushindi.

 Hata hivyo alisema baada ya kupoteza mchezo huo wanajipanga kwa ajili ya kujiandaa na michezo mingine inayokuja ambapo mchezo ujao watacheza na Gwambina.

“Timu yangu haikuwa na tatizo lolote lilifanya tukose ushindi lakini ndio tunaogopa kuongea, ila kiukweli kama sio waamuzi basi hawa Yanga walikuwa wanatuachia pointi tatu.

“ Sisi tulipanga kuumaliza mchezo ule ndani ya dakika 45 tu sema ndio haikuwa kama ambavyo tulitaka,” alisema.