NA MWANDISHI WETU

AMRI Said, aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Mbeya City amefutwa kazi Oktoba 20 baada ya timu kutokuwa na mwendo mzuri msimu wa 2020/21.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Mathias Wandiba ambaye ataendelea kuwa msimamizi wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu Bara.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa juzi kukaa kwenye benchi na timu ya Mbeya City ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.

Kwa msimu wa 2020/21, Mbeya City imejenga ufalme wake nafasi ya 18 kwa kuwa imedumu kwa muda wa raundi saba mfululizo.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi saba kibindoni ina pointi mbili kwa kuwa ilipata sare mechi mbili ndani ya ligi na kupoteza jumla ya mechi tano.

Safu yake ya ushambuliaji iliweza kufunga bao la kwanza juzi Oktoba 20 wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.