NA MWANDISHI WETU

YANGA inashuka dimbani kesho kucheza mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na kocha mpya Cedric Kaze, huku ikiwa haina uhakika wa kuwatumia wachezaji wake wawili kwenye mchezo huo.

Wachezaji wawili ambao wanaweza kuukosa mchezo huo ni  Ally Makame na Mapinduzi Balama, mchezo utakaopigwa Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Polisi Tanzania.

Makame kwa mujibu wa mmoja ya viongozi wa timu hiyo  anasumbuliwa na malaria huku Balama akiendelea kutibu majeraha yake ambayo aliyapata mwishoni mwa msimu uliopita wa 2019/20.

Kwa sasa taryari Balama ameanza mazoezi mepesi ili kujiweka sawa  kinachosubiriwa ni ripoti ya doktari kujua kwamba kama anaruhusiwa kuanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake.

Balama msimu uliopita alifunga jumla ya mabao matatu kwenye ligi na bao lake alilomtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula liliingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya bao bora kwa msimu wa 2019/20.

Alifunga bao hilo Januari 4, kwenye dabi ambapo dakika 90 zilikamilika kwa timu hizo kutoshana kwa kufungana mabao 2-2, Uwanja wa Mkapa.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Polisi Tanzania, Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa kwenye mbio za kusaka pointi tatu muhimu.

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi sita  ikiwa na pointi 11.