WAKATI janga la corona lilipoanza kuivamia dunia likitokea Wuhan nchini China, wataalamu wengi wa afya walibashiri kwamba watu barani Afrika watakufa kama kuku wa mahepe.

Walitoa sababu mbalimbali ikiwemo nchi nyingi katika bara hilo kuwa na mifumo mibovu na dhaifu ya afya, kutokuwa na mindombinu mizuri katika sekta ya afya pamoja na tamaduni za kiafrika zinaweza kuchangia kasi ya maambukizi kuwa kubwa.

Kwa wastani, ugonjwa wa corono iliiingia Afrika manamo mwezi Machi mwaka 2020, baada ya miezi mitatu kuzuka nchini China kuvamia baadhi ya nchi za mashariki ya kati, kuelea Ulaya.

Baada ya Afrika ugonjwa huo ukaelekea Marekani na eneo zima la nchini za Latini ambapo huko ugonjwa huo umevuruga sana kiasi kwamba kwa mujibu wa takwimu Marekani ndiyo nchi inayoongozwa kwa vifo vingi na watu walioambukizwa.

Barani Afrika mambo hayakwenda kama yalivyotabiriwa, ambapo bara hili inasemekana ndilo lililoathirika kwa kiasi kidogo pamoja na kutokuwa na mindombinu ya kisasa kwenye mifumo ya afya.

Bara hilo lenye idadi ya watu zaidi ya bilioni moja, lina watu milioni 1.5 ambao wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona, kwa mujibu wa data iliyokusanywa na Chuo Kikuu cha John Hopkins University.

Afrika nzima iliandikisha jumla ya vifo karibu 37,000 ikilinganinshwa na karibu vifo vya watu 58,000 huko Amerika, watu 230,000 barani Ulaya na 205,000 barani Asia.

Ukiangalia takwimu hizo utabaini kwamba idadi ni ya chini kuliko za Ulaya, Asia au Amerika, huku kukiwa na taarifa katika baadhi ya nchi hasa barani Ulaya zikikumbwa na wimbi la mara ya pili la maambikizi ya corona.

“Takwimu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa corona barani Afrika zinaashiria kuwa havijaathiri sana watu katika bara hilo,” kulingana na utafiti wa pamoja uliofanywa kubaini jinsi mataifa yalivyoshughulikia janga la corona PERC, ulioleta pamoja mashirika kadhaa ya kibinafsi na ya umma.

Viwango vya chini vya upimaji wa watu katika baadhi ya nchi za Afrika unaendelea kuwa kikwazo katika juhudi za kukabiliana na janga la corona huku idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na Covid-19 vikikosa kunakiliwa, alisema Dk. John Nkengasong, Mkuu wa Afrika wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC).

Katika utafiti wa wataalamu hao umebaini saabu zilizochangia kwanini viwango vya corona vimekuwa vidogo barani Afrika ikiwa ni pamoja na hatua za haraka zilizochukuliwa na nchi hizo.

Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona katika bara la Afrika kilithibitishwa nchini Misri Februari 14 mwaka huu na kulikuwa na hofu virusi hivyo vipya huenda vikaathiri watu vibaya kutokana na mifumo duni ya afya katika nchi nyingi barani humo.

Hatahivyo, nchi za Afrika zilichukua hatua za dharura kudhibiti virusi kuenea kwa haraka. Muongozo wa afya ya umma ikiwa ni pamoja na kutosalimiana kwa mikono, kunawa mikono mara kwa mara, watu kutokaribiana na kuvaa barakoa- ulibuniwa.

Baadhi ya nchi kama vile, Lesotho ilianza kuchukua hatua ya kuzuia maambukizi hata kabla ya mtu yeyeyote kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Ilitangaza hali ya dharura na kufunga skuli zote Machi 18, na kuweka amri ya kutotoka nje kwa kwa wiki tatu na siku 10 baadaye kama hatua ya kushirikiana na nchi zingine za Afrika katika juhudi za kukabiliana na jana la corona

Lakini amri ya kutotoka nje ilipoondolewa mapema mwezi Mei, Lesotho ikatangaza mgonjwa wake wa kwanza wa corona.

Nchi hiyo ambayo ina watu zaidi ya milioni mbili kufikia sasa, imethibitisha kuwa na watu 1,700 walioambukizwa virusi huku watu 40 wakifariki kutokana na ungojwa wa Covid-19.

Utafiti uliofanywa na PERC katika nchi 18 mwezi Agosti PERC, unaonesha msaada wa umma kwa hatua za usalama ulikuwa, huku asilimia 85 ya walioshiriki utafiti huo wakisema kuwa walivalia barakoa wiki iliyotangulia.

“Kutokana na utekelezaji wa muongozo wa afya ya umma na msaada wa kijamii, nchi wanachama wa muungano wa Afrika zilifanikiwa kudhibiti virusi vya corona kati ya mwezi Machi na Mei,” ripoti ilisema.

Pia uliongezea kwamba ” kulegezwa kiasi kwa masharti katika miezi ya Juni na Julai kulishabikiana na ongezeko la viwango vya maambukizi ya virusi vilivyoripotiwa katika nchi tofauti barani Afrika”.

Kutoka wakati huo, viwango vya maambukizi na idadi ya vifo vimeonekana kushuka katika bara hilo, hali ambayo inahusishwa msimu wa baridi kali.

Kutekelezwa kwa masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kulikuja na changamoto zake. Watu walipoteza ajira kwa kiwango kikubwa.

Afrika Kusini ambayo ni moja ya nchi iliyoweka masharti makali duniani-, jumla ya ajira milioni 2.2 zilipotezwa nusu ya kwanza ya mwaka.

Nchi kadhaa zimelazimika kufungua chumi zao licha ya idadi ya maambukizi bado kuwa juu kuliko ilivyokuwa kabla ya kutolewa kwa amri ya kutotoka nje.

Kulingana na ripoti ya PERC, watu walikuwa na maoni tofauti kuhusu hatua ya nchi kurejelea shughuli za kiuchumi, watu sita kati ya kumi walitaka uchumi ufunguliwe na wanaamini hatari ya kupata maambukizi itakuwa chini ikiwa watu watazingatia muongozo wa afya ya umma utazingatiwa.

Hata hivyo, watu saba kati ya kumi wanafikiria kurejelea kwa hali ya kawaidi kunawatia hofu.

Nchi nyingi za Afrika zina idadi kubwa ya vijana kuliko wazee hali ambayo huenda ilichangia pakubwa kudhibiti maambukizo ya Covid-19.

Kimataifa, watu wengi waliofariki kutokana na corona wana miaka 80, wakati Afrika ina idadi kubwa ya vijana walio na miaka 19, kwa mujibu wa data za Umoja wa Mataifa.

”Janga hilo halijaathiri watu walio na umri mdogo…karibu asilimia 91 ya maambukizo ya virusi katika eneo la kusini mwa Jangwa la corona ilikuwa ni ya watu walio chini ya miaka 60 na zaidi ya asilimia 80 ni ya wale ambeo hawaoneshi dalili”, limesema Shirika la Afrya Duniani (WHO).

Afrika ina karibu asilimia tatu ya watu walio na zaidi ya miaka 65 ikilinganishwa na Ulaya, Amerika Kaskazini na nchi tajiri za bara Asia zilizo na idadi kubwa ya wazee.

“Moja ya sababu iliyochangia idadi kubwa ya maambukizo ya virusi vya corona katika nchi za magharibi ni kwamba wazee walikuwa wanaishi katika makazi maalumu na suala hilo lilisababisha virusi kusambaa kwa kasi”, alisema Dk Moeti.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Maryland nchini Marekani ulibaini uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa na kusambaa kwa maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19.

“Tulichunguza mambo ya awali katika miji 50 duniani. Na tulibaini kuwa virusi vilisambaa kwa urahisi katika maeneo yaliyokuwa na viwango vya chini vya joto” alisema Mohammad Sajadi, mtafiti mkuu.

“Sio kwamba virusi havisambai katika mazingira mengine yaliyo na hali ya joto, lakini virusi vinasambaa kwa haraka viwango vya joto vikishuka.” Viwango vya maabukizi viliongezeka kwa kasi nchini Afrika Kusini msimu wa baridi kali.

Lakini hali ya hewa ilipobadilika, idadi ya watu walioambukizwa virusi vilishuka, hali iliyobadili mtazamo wa bara, kwasababu Afrika Kusini inachangia karibu nusu ya idadi ya maambukizi na vifo ya corona barani Afrika.

Janga la Covid- 19 lilikuja wakati ambapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa bado inashughulikia mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa ebola.

Nchi jirani zilikuwa zimeweka mikakati kabambe ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufanya uchunguzi wa afya kwa wasafiri hasa wanaoshukiwa kuwa na Ebola, hali ambayo ilikuwa rahisi kujumuisha Covid-19

Nchi kadhaa za Afrika Magharibi zilikuwa zikikabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola kutoka mwaka 2013-16 – pia zilikuwa zimepata uelewa wa jinsi ya kuzuia Covid-19, ikiwa ni pamoja na kuwatenga watu walioambukizwa.

Pamoja na hilo wahudumu wa afya nchini Nigeria, ambao walikuwa wakizunguka vijijini kuwapa watoto chanjo ya polio walichukua nafasi hiyo kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa mpya wa corona.

Kwa hivyo, japo miundo mbinu katika nchini nyingi za Afrika haijaimarika ikilinganishwa na maeneo mengine duniani, nguvu ya bara hilo iko katika mifumo yake ya afya ya jamii inapoyopambana na kuwapa usalama watu wake licha ya changamoto zilizopo.

Licha ya juhudi hizo nchi za Afrika hazistahili kurudi nyuma katika mapambano dhidi ya corona.