ZASPOTI
KOCHA, Frank Lampard, amesema, mshambuliaji wa kimataifa wa Morocc, Hakim Ziyech, anaweza Chelsea katika kiwango chengine baada ya kutua Stamford Bridge.


Uhamisho wa majira ya kiangazi wa winga huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Ajax ulitangazwa mnamo Februari, na Ziyech alijitokeza katika mechi ya kwanza ya kirafiki ya sare ya 1-1 dhidi ya Brighton mnamo Agosti.


Mechi ya mwisho ya ushindani ya klabu ya Ziyech ilikuwa mwezi Machi na Ajax, ikimuacha bosi wa ‘Blues’ Lampard bado ana hamu na winga huyo mbunifu kuelekea hali ya ukamili wa mechi.
Alipoulizwa ikiwa Ziyech anaweza kuongeza makali na kuipeleka Chelsea muonekano mpya, Lampard alijibu: “Ndio, na nadhani kuna mchanganyiko wa vitu.


“Ikiwa unaleta wachezaji, kila wakati unatafuta kujenga uhusiano kote uwanjani iwe ni beki kamili na mawinga, washambuliaji na watu wanaocheza nyuma yao.(Goal).