LONDON

KOCHA Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard, amesema kupoteza mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs kumemvuruga kwa kuwa walipaswa kuibuka washindi.

Mchezo huo wa Kombe la Carabao hatua ya 16 bora uliochezwa usiku wa kuamkia jana, Chelsea ilianza kushinda ndani ya dakika 45 za mwanzo kabla ya wapinzani wao kusawazisha na kupelekea kumalizika kwa sare ya bao 1 – 1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa njia ya penalti.

Timo Werner alianza kuifungia mamo dakika ya 19 Chelsea bao lililodumu hadi katika dakika ya 83 Erik Lamela alipoipatia bao la kusawazisha Spurs inayonolewa na Jose Mourinho ambapo kwenye penalti, ilishinda penalti 5 – 4 baada ya

Mason Mount kukosa penalti kwa upande wa Chelsea.

“Tulikiwa tunahitaji kubaki kwenye ushindani ila inaonekana wachezaji wangu walikuwa wamechoka, kwa hali ile ilikuwa ngumu kupata matokeo chanya na ilikuwa ni ngumu kwetu kupoteza kwa kuwa tulianza kushinda,” alisema nahodha huyo wa zamani wa klabu hiyo.