NA MWAJUMA JUMA

LIGI kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa kuanza Novemba 7, mwaka huu.Ligi hiyo ambayo itashirikisha timu 12, itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu wa Kamati ya Mashindano Hussein Ahmada Vuai, alisema ligi hiyo itachezwa katika viwanja vya Mao Zedong, Gombani na Amaan kama utakuwa umeshamalizika matengenezo yake.

Alisema  mpaka sasa matarajio yao kuwa ligi hiyo itaanza  muda huo, kama ambavyo kalenda ya Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar ZFF linavyoonyesha.

“Ligi itaanza Novemba 7, mwaka huu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kama ambavyo kalenda ya Shirikisho letu inavyoelekeza”, alisema.