NA AHMED MAHMOUD 

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, amesema kuwa serikali atakayoingoza itajali haki utu sanjari na kuendeleza haki za binadamu na demokrasia ikiwemo kuendeleza mchakato wa katiba mpya.

Akiongea kwenye mkutano huo katika viwanja vya Kilombero, Prof. Lipumba, alisema kuwa bado wananchi wengi ni maskini wa kipato huku mazingira rafiki yakiwa hayajawekwa sawa kufanya biashara na uwekezaji.

Alisema wengi wao wamepigika kisawa sawa huku wapewa kiparata cha 20,000 kutembea nacho wakati hakuna mazingira wezeshi..

“Utakuta mama anazunguka na vitumbua mchana kutwa sio watu hawana hamu navyo fedha ndio changamoto kubwa na mzangira ya wajasiriamali yamesahauliwa” alisema.

Alitanabaisha kuwa serikali itakayoongozwa na chama hicho pindi akipewa ridhaa itajali na kuangalia mazingira rafiki ya uwekezaji utakaosaidia kuondoa changamoto ya maeneo ya wafanyabiashara hao, ili kuongeza wigo wa ulipaji kodi.

Mgombea Ubunge kupitia chama hicho, Magdalena Shangay, alisema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa jiji la Arusha kuacha ushabiki na maisha yao na kumchagua yeye kuwa Mbunge ili kubadilisha Arusha.