MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, amesema, kikosi chake lazima kifikie hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya Euro mwakani.

Timu ya taifa ya Ujerumani ilitoka sare ya bao 3-3 dhidi ya Uswisi kwenye mchezo wa michuano ya UEFA Nations League, ikiwa sare nne kwa mabingwa hao wa dunia mara nne.

Katika michezo mitano ya mwisho waliocheza, wameshinda mchezo mmoja tu,Licha ya kikosi hicho kuwa na mapungufu katika mchezo huo hususani eneo la ulinzi, baada ya mechi kumalizika, Low, alisema walifanya makosa kadhaa kwenye safu ya ulinzi, lakini wanahitaji kurekebisha makosa hayo.

Sasa Ujerumani wanashika nafasi ya pili kwenye kundi namba 4 wakiwa na pointi sita, tofauti ya pointi moja dhidi ya vinara, Hispania yenye pointi saba.(Goal).