NEW DELHI, INDIA

IDADI  ya maambukizi ya virusi vya corona imepindukia milioni 40 kote ulimwenguni.

Kulingana na Chuo Kikuu cha John Hopkins ambacho kinakusanya takwimu kutoka kote duniani, idadi hiyo ilipindukia wiki iliyopita.

Aidha wataalamu walisema idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo.

Hadi sasa, zaidi ya watu milioni 1.1 wamefariki kutokana na virusi vya corona, ingawa wataalamu pia wanaamini idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo.

Marekani, India na Brazil ndiyo mataifa yanayoripotiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ulimwenguni kote.

Hata hivyo, ongezeko la kimataifa la maambukizi la wiki za hivi karibuni limekuwa likishuhudiwa zaidi barani Ulaya, ambako zaidi ya watu 240,000 wamefariki kutokana na janga hilo hadi sasa.