BANGKOK,THAILAND

MAELFU ya raia wa Thailand wamefanya maandamano dhidi ya Serikali katika miji 20, licha ya mvua na hata kukamatwa kwa wanaharakati kadhaa .

Kwa mujibu wa kundi la mawakili wa Thailand wanaotetea haki za binadamu, wanaharakati saba walikamatwa baada ya maandamano ya Bangkok kumalizika kwa amani.

Kiongozi mmoja mkuu wa maandamano hayo Panupong Jadnok alikamatwa na maofisa wa usalama waliomuonesha waranti wa kutaka akamatwe.

Maandamano hayo ambayo yaliingia siku ya tano mfululizo, yanalenga kuishinikiza Serikali ya Waziri Mkuu Prayuth Chan kujiuzulu, kuandikwa katiba mpya na mageuzi katika utawala wa kifalme nchini humo.

Kulingana na kundi la mawakili wa kutetea haki za binadamu, tangu Oktoba 13 polisi walitoa waranti wa kutaka wanaharakati 76 wakamatwe.