NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Machicha FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Coco Sport Ndondo Cup, baada ya kushindwa kwa mikwaju ya penalti 3-2, dhidi ya Team Prince kwenye mchezo wa fainali.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Kiembe Samaki majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa na mashabiki wengi.

Hadi  mchezo huo unamalizika hakuna timu iliofanikiwa kuzifumua nyavu, ambapo sheria ya kupigiana mikwaju ya Penalti ikatumika ili kupatikana bingwa.

Kwa matokeo hayo timu ya Machicha ilipata penalti tatu kupoteza mbili na Team Prince kupata mbili na kupoteza tatu.

Bingwa wa mashindano hayo alijinyakulia  shilingi milioni 8,000,000, kombe,medali ,seti ya jezi na ngao,huku mshindi wa pili alijinyakulia milioni 4,000,000,medali,seti ya jezi.