PARIS,UFARANSA

MAELFU ya watu wamendamana nchini Ufaransa kumuunga mkono Samuel Paty, mwalimu aliyekatwa kichwa kwa kuonesha wanafunzi picha ya Mtume Muhammad.

Waandamanaji hao walikusanyika kwa pamoja eneo la Bellecour, ili kutoa heshima zao za mwisho huku wengine walijitokeza mjini Nantes, Toulouse, Strasbourg, Marseille na Bordeaux.

Watu 11 walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi, huku ikiwa hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu kukamatwa kwao.

Ndugu wanne wakaribu wa washukiwa walishikiliwa kwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.

Watu wengine sita walishikiliwa, akiwemo baba wa wanafunzi ambaye alitambulishwa na vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa alikuwa muhubiri na muislamu mwenye itikadi kali.

Mauaji hayo yanakuja baada ya shambulio la mwaka 2015 la Charlie Hebdo -ambalo lililengwa na washambuliaji kwa kuchapisha katuni za Mtume Mohammad.