NA MWAJUMA JUMA

UONGOZI wa timu ya soka ya Mafunzo umesema kuwa unajipanga kuhakikisha msimu mpya wa ligi timu hiyo inafanya vizuri zaidi na kutwaa ubingwa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa idara ya Michezo ya Jeshi hilo Khamis Ali Machenga alipozungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Kilimani.

Alisema  msimu uliopita timu yao haikuweza kutwaa ubingwa kutokana na sababu mbali  mbali ikiwemo kutokuwa naaandilizi mazuri.

Mafunzo ambayo inashiriki ligi kuu ya Zanzibar katika msimu uliopita iliibuka katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo, ambapo msimu huu wanataka kuondokana na nafasi hizo.

“Msimu huu tunajipanga ili kuona kwa kiasi gani tunaifejesha ile Mafunzo ambayo iliyotamba katika miaka ya nyuma”, alisema.

Hata hivyo alisema miongoni mwa mipango yao ambayo wanaona watafanikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kupambana.

Alisema  katika usajili wa msimu huu wamesajili wachezaji wengi vijana na kuchukuwa wale ambao wana uwezo na kuhimili mikikimikiki ya ligi hiyo.

Katika msimu wa 2019/2020 timu ya Mlandege ndio iliyoibuka kuwa bingwa kwa kujikusanyia pointi 68 kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo Zimamoto walikuwa wa pili.