LONDON, England
NAHODHA wa Manchester United, Harry Maguire, amezoza na mshambuliaji, Marcus Rashford kutokana na kadi ya njano aliyoonyeshwa, Erik Lamela.

Lamela alionekana kama alianza kumpiga Anthony Martial, jambo ambalo liliamsha hasira za mchezaji huyo wa Ufaransa ambaye alirudishia na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mwamuzi wa mchezo kati ya United na Spurs, alimuonyesha kadi nyekundu Martial, lakini, Lamela alioneshwa ya njano, katika mchezo ambao Spurs ilikilaza kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer magoli 6-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Katika tuki hilo, ambalo lilinaswa na kamera pamoja na sauti zao zikisikika kwa nahodha, Maguire, akibishana na Rashford juu ya kama Lamela naye kuonyeshwa kadi nyekundu au laa.
Rashford alisikika akimlaumu nahodha wake kwa kushindwa kulisimamia hilo akisema: “Hakuna lolote juu ya kiwiko alichopiga (Lamela)?

Aliuliza mshambuliaji huyo baada ya mwamuzi, Anthony Taylor kumfuata Lamela na kutoa kadi ya njano.Rashford aliendelea: “Kwanini na tukio na matukio yanafanana?” Maguire akamjibu: “Siyo kama lile, wameangalia katika VAR.”
Lakini Rshford alisisitiza: “Amempiga kiwiko!’ Na nahodha wake alimaliza kwa kumwambia: “Wameangalia na hakuna hilo.(Goal).