NA KHADIJA WAZIRI, MAFIA

MJUMBE wa Kamati Kuu Taifa, ambae Waziri Mkuu Nchini, Kassim Majaaliwa, ametoa agizo la kuletwa meli nyingine ya kusafirisha abiria baada ya wanayosafiria kufanyiwa marekebisho.

Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kilindoni kisiwani humo “kwa kuwa meli mnayosafiria imepandishwa juu kwa lengo la kufanyika ukarabati tutawaletea meli ya jeshi iwasaidie kwa muda hadi itakapo maliza matengenezo meli yenu” Alisema Kassim Majaaliwa. 

Meli hiyo, imeshaanza  safari zake za kwenda Nyamisati na kurudi Mafia kwa lengo la kuwasafirisha wananchi wa kisiwa hicho  ikiwa imekabidhiwa halmashauri ya Wilaya mafia.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa meli hiyo, Mkuu wa Wilaya Mafia, Shaibu Nnunduma  ameishukuru serikali kuu kwa kuona umuhimu wa wananchi wa Mafia na kuwafikishia usafiri wa uhakika huku akiwataka wananchi kutumia vizuri usafiri huo na kuutunza hadi pale meli ya MV Captain One kumalizika ukarabati wake.   

Sambamba na hayo nao baadhi ya wasafiri na wasafirisha bidhaa zao walisema usafiri huo ni mzuri na wenye uwezo wa kuwaongezea kipato katika harakati zao za biashara kutokana kusafirisha mizigo yao ikiwa salama tofauti na siku mbili zilizopita mara baada ya MV Captain One kupata dharura.